Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na wajumbe wa
Baraza la Usajili wa Wataalam wa Afya ya Mazingira nchini, leo
wakati wa uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi , akimkabidhi cheti cha
usajili wa utaalamu wa afya ya mazingira, Mary Swai ambaye ni
Mwenyekiti mpya wa awamu ya pili ya Baraza la Usajili wa Wataalam
wa Afya ya Mazingira nchini, leo wakati wa uzinduzi wa baraza hilo
jijini Dar es Salaam.
Frank John na Hassan Silayo- Maelezo
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi amewataka wajumbe wa
Baraza la Usajili wa Wataalam wa Afya ya Mazingira nchini, kufanya
kazi kwa kujituma na ushirikiano ili kupambana na changamoto
zinazokabili sekta hiyo na kuzuia maambukizi ya magonjwa.
Dk.
mwinyi ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika
jana jijini Dar es salaam ambapo alisema sekta ya afya na ustawi wa
jamii inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ongezeko la milipuko ya
magonjwa kutokana na uchafuzi wa mazingira.
Amebainisha
kuwa afya ya mazingira ni suala mtabuka ambalo linahitaji
ushirikishwaji wa wadau wa sekta ya afya ya mazingira ili kutoa matokeo
yenye tija na ubora wa hali ya juu katika kupambana na magonjwa hayo.
Ameongeza
kuwa serikali inatarajia kwamba kwa kutumia baraza hilo huduma ya afya
ya jamii itatolewa kwa wananchi kwa viwango vinavyotakiwa na hivyo,
kuboresha maisha ya wananchi kwa kusimamia na kudhibiti utoaji wa huduma
ya afya ya mazingira kwa misingi ya haki.
“Pia
wataalam wa kada hii watajiendeleza na kufikia kiwango cha juu cha
elimu tofauti na miaka iliyopita ampapo wengi waliridhika na kubaki
katika eneo moja kwa muda mrefu na kusababisha kudumaa kwa
taaluma,amesema Dk.Mwinyi.
Amesema
kwa kufanya , hivyo upo uwezekano mkubwa wa kupunguza ongezeko la
kasi ya magonjwa, vifo na madhara mengine katika jamii yatapungua
ikiwa huduma ya afya ya jamii itaboreshwa.
Naye
Mwenyekiti wa baraza hilo , lililomaliza muda wake Bwana Fabian Magoma
alisema linakabiliwa na changamoto za upungufu wa fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa shughuli za baraza na ukosefu wa mitaala hivyo linahitaji
ushirikiano wa karibu na taasisi zinazoandaa mitaala ya elimu nchini.
Magoma
alishauri baraza hilo, liangalie sheria zinazohusiana na afya ya
mazingira, ili waweze kutambua taaluma hiyo. Huku akiongeza kuwa watu
wanaoteuliwa kufanya kazi hiyo wawe ni wa kada hiyo.
Kwa
upande wake mjumbe wa baraza jipya Haji Mdemu alishauri serikali
kuzingatia mbinu za zamani za afya mazingira , kuzifufua ili kuimarisha
afya mazingira na uwajibikaji wa maafisa afya.
Baraza
hilo lilizinduliwa rasmi mwaka 2009 ikiwa ni matokeo ya sheria ya
kusajili wataalam wa afya mazingira ya mwaka 2007 iliyopitishwa na Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiwa na majukumu ya kusajili,
kudhibiti nidhamu kiutendaji katika kada ya afya ya mazingira pamoja na
kumshauri waziri husika juu ya masuala yote yahusuyo afya ya mazingira
nchini.
No comments:
Post a Comment