Picha na MAELEZO- Dar es salaam
Na Mwandishi wetu, MAELEZO-Dar es salaam
Japan imeipatia Tanzania imepata mkopo wa shilingi bilioni 54.13 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji mpunga ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo hapa nchini.
Makubaliano hayo yametiwa saini jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada ampapo Wilaya 80 zinazolima mpunga hapa nchini zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo.
Akizungumza mara ya kusaini makubaliano hayo Khijjah alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kukarabati miundo mbinu ya zamani ya umwagiliaji na kujenga miundo mbinu mipya ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo hapa nchini.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni kupunguza uagizaji wa mchele kutoka nje ya Tanzania Japan ikiwemo badala yake wananchi wajikite katika kuzalisha hapa nchini bila ya kutegemea mvua.
Aliongeza kuwa mpango ni sehemu ya Mkakati wa Serikali wa Kupunguza umaskini kwa wananchi na kukuza uchumi na hivyo kuboresha maisha ya wanachi kwa kuwahakikishia upatikanaji wa chakula cha kutosha.
Aidha Katibu Mkuu huyo alisema kuwa chini ya mkopo utasaidia kuongeza uzalishaji kutoka tani 3-4 kwa hekta hadi kufikia tani 6 katika mvuno mmoja.
Alimhakikishia Balozi wa Japan kuwa Serikali itahakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Naye Balozi wa Japan nchini Masaki Okada alisema kuwa karibu asilimia 75 ya Watanzania wamejiajiri katika sekta ya kilimo na hivyo fedha hizo ni muhimu kwa Tanzania katika kutekeleza malengo yake iliyojiwekea katika Kilimo kwanza.
No comments:
Post a Comment