Sunday, 25 August 2013

ANGALIA PICHA ZA KIKAO CHA NEC DODOMA


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ana Makamu wake (Zanzibar) Dk. Ali Moahammed Shein wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, baada ya kuzindua baraza hilo leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Kinana.


 Mwenyekiti wa Baraza la Ushsuri la Viongozi wastaafu wa CCM, Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongoza kikao cha kwanza cha Baraza hilo leo mjini Dodoma. Kushoto ni Wajumbe wa Baraza hilo John Malecela na Amani Abeid Karume na kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Benjamin Mkapa na Katibu wa Baraza Pius Msekwa.


 Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao chca NEC kilichofanyika leo mjini Dodoma kama Baraza la Kitaifa la Kitaasisi kujadili maoni ya rasimu ya katiba mpya yaliyotolewa na mabaraza ya chini ya kitaasisi ya CCM hivu karibuni. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Sheni na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana


 Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa kwenye kikao hicho


 Wajumbe wa Baraza la Ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, Kutoka kulia, John Malecela, Amani Abeid Karume na Pius Msekwa wakiwa kwenye kikao cha NEC, baada ya Baraza hilo kualikwa kwa ajili ya kushiriki katika mjadala wa rasimu ya Katiba mpya kwa upande wa CCM kama taasisi.


 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro akiwasilisha makusanyo ya maoni ya katiba kama yaliyotolewa na mabaraza ya ngazi za chini ya CCM kama taasisi, leo kwenye kikao hicho cha NEC.


   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana mambo na watendaji wenzake katika Chama, nje ya ukumbi wa White House mjini Dodoma leo, kabla ya kuzinduliwa Baraza la Ushauri la Wastaafu wa CCM . Kutoka kulia ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhamed Seif Khatib, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Abdallah Bulembo.


 Karibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimshauri Jambo Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa Baraza la ushsuri la Wastaafu wa CCM leo mjini Dodoma.


 Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika uzinduzi wa Baraza hilo


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia mmoja wa wana-CCM waliohudhuria hafla ya kuzinduliwa Baraza la Washauri la Wastaafu wa CCM leo mjini Dodoma


 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Hamis akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Martine Shigela wakati wa kikao cha NEC mjini Dodoma


 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Buhiye akiwa katika ukumbi wakati wa kikao cha NEC leo mjini Dodoma









Katibu wa NEC, Itrikadi na uenezi Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu yaliyojiri katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika jana. Pamoja na mambo mengine, Nape amesema, Kamati Kuu amejadili suala ya sakata la madiwani wanane katika Halmashausri ya Bukoba, mkoani Kagera ambao Halmashauri Kuu ya CCM mkoa huo ilutangaza kuwatimua hivi karibuni ambapo Nape amesema, Kamati Kuu imeamua kuwaita ili kukutana nao kesho viongozi wanane katika mloa huo aliowataja kuwa Mwenyekiti na Karibu wa CCM mkoa wa Kagera, Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba mjini, Mbunge wa Bukoba mjini na Meya wa Halmashauri ya Bukoba. IMETAYARISHWA NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...