Thursday, 29 August 2013

TASWIRA YA MWENGE WA UHURU WAINGIA MKOA WA PWANI

Mwenge wa Uhuru ukiwa mpakani mwa Mkoa wa Morogoro na Pwani leo tayari kwa makabidhiano ya Mwenge huo uliomaliza ziara yake mkoani morogoro na Kuanza ziara Mkoa wa Pwani mara baada ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa morogoro kwa lengo la kukagua na kufungua miradi na shuguli za Maendeleo Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris wakati wa Shamra shamra za Mbio za Mwenge wa Uhuru uliomaliza ziara yake Mkoani Morogoro Leo.
Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika makabidhiano hayo leo.









Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika Mapokezi hayo leo

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera  akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh Mwamtumu Mahiza leo mara baada ya mwenge huo kumaliza ziara yake mkoa wa morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh Mwamtumu Mahiza akipokea Mwenge wa Uhuru 

Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mh Dk Shukuru Kawambwa  akiwa na Naibu Waziri wa Afya Seif S Rashid wakiwa katika Mapokezi hayo




No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...