Wakati msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ukielekea Wilayani Missenyi kukagua sehemu utakapojengwa uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Omukajunguti, gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 570 BYU lilowabeba Waheshimiwa Wabunge 11 lilipata hitilafu na kutaka kuungua.
P.T
Ajali hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu kilometa moja kutoka mpakani mwa Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi ambapo gari hilo aina ya costa lilianza kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma wakati likiwa kwenye mwendo mkali na kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo ndani ya gari hilo.
Kwa mujibu wa wabunge waliokuwemo kwenye gari hilo, baada ya kuambiwa kuwa gari linaungua kila mmoja alifanya juhudi za kujiokoa, wengine wakipitia madirishani.
Kwa Bahati hakuna Mbunge aliyeumia isipokuwa Mhe. Batenga aliumia mkono kidogo baada ya kubanana sana mlangoni.
Baada ya kila mmoja kutoka gari hilo liliendelea kutoa moshi mzito sana lakini kwa halikushika moto na baadae lilizimika na kuacha kutoa moshi.
Wabunge waliokuwemo katika gari hilo ni Rebbecca Mngondo (Arusha Viti Maalumu), Rita Kabati (Iringa Viti Maalumu), Mariam Msabaha (Zanzibar Viti Maalumu), Mhe. Batenga (Kagera Viti Maalumu), Mhe. Madabida (Dar es Salaam Viti Maalum), Clara Mwatuka (Mtwara Viti Maalumu).
Wengine ni Mzee Hussein (Zanzibar), Mussa Haji Kombo (Pemba Zanzibar), Abdul Mteketa (Jimbo la Kilombelo), Mutula Mutula (Jimbo la Tunduru Kusini).
Aidha Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Peter Serukamba Hakuwemo katika gari hilo lilotaka kuungua.
No comments:
Post a Comment