MOROGORO KUSINI


MSAFARA WA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI ULIPOKEREWA HIVI NA VIJANA WA KIKUTU KIJIJI CHA KONGWA.

 
 
WANANCHI WA KABILA WAKUTU WA KIJIJI CHA KONGWA TARAFA YA MVUHA WILAYA YA MOROGORO VIJIJINI NDIVYO WALIVYOUPOKEA MSAFARA WA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI INNOCENT KALOGELIS WAKATI WA KUTATUA MGOGOLO WA WAFUGAJI NA WAKULIMA WA KIJIJI HICHO NA VITONGOJI VYAKE JANA SEPTEMBA 3, 2011. 



WANANCHI wenye hasira kali zaidi ya 80 wakazi wa kijiji cha Kongwa kabila la Wakutu Tarafa ya Mvuha wilaya ya Morogoro Vijijini wamechoma moto nyumba saba za wafugaji wa jamii ya kisukuma baada ya wafugaji watatu kudaiwa kulisha mazao aina mbalimbali kwa kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima na kuwajeruhi kijijini hapa agosti 28 na septemba 3 mwaka huu mkoani hapa. 




Katika tukio hilo wafugaji wanne na watoto watano walikamatwa kutokana na vurugu hizo katika eneo la kitongoji cha Lukoni ambapo familia ya mfugaji Bangili Mwanabahati akiwemo mama yake mzazi na watoto watano walikamatwa na msafara wa mbunge wa jimbo la Morogoro kusini huku vijana watatu wa wafugaji wakituhumiwa kwa kupiga wakulima hao wakati wa matukio ya kulisha mifugo katika mashamba mbalimbali ya wakulima kijijini hapa. 




BLOGU HII ilishuhudia Vijana hao walipelekwa katika kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro ambapo familia ya mfugaji Bangili Mwanabahati walihifadhiwa katika mji mdogo wa Mvuha kwa ajili ya usalama wa maisha yao chini ya Katubu Tarafa wa Mvuha. 




Akizungumza katika kijiji cha Kongwa na wananchi wenye hasira kali mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogelis aliwaambia wananchi hao walikuwa na silaha za jadi kuwa msafara wao umefika kijijini hapo kwa lengo la kutatua mgogolo uliopo kati ya wakulima na wafugaji na kuwataka kutulia kwani tayari suala hilo litapatiwa ufumbuzi. 




Kalogelis alisema kuwa taarifa za mgogolo ambao una daiwa kuanzishwa na wafugaji kwa kulisha mifugo katika mashaamba ya wakulima taarifa hizo tayari zimefika katika uongozi wa juu wa serikali na kamati ya ulinzi na usalama ipo katika hatua za mwisho za kulishughulikia mgogolo huo. 




Mbunge huyo alisema kutokana na wafugaji hao kudaiwa kuingia kijijini hapo mifugo bila ya kuafuata taratibu za kisheria jana wananchi wa kijiji hicho walifanikiwa kukamata ng'ombe 125 huku kibali chao kikionyesha wanafarishwa kutoka Dodoma na kwenda Dar es Salaam lakini walipofika mkoa wa Morogoro walibadilisha uamuzi huo na ng'ombe hao kuingizwa katika ardhi ya kijiji hicho cha Kongwa mali ya Msalali Muwila ambapo kamati ya ulinzi ya wilaya ya Morogoro inamsaka mmiliki wa ng'ombe hao ili awaondoe katika wilaya hiyo. 





Katika msafara huo ambao ulifika kijijini hapo majira ya saa 4:50 asubuhi ulipokewa na vijana wenye hasira kati ya rika ya umri wa miaka 12 na 25 huku wakiwa na silaha za jadi mikuki, panga, shoka, visu, rungu na majembe ambapo waliadhimiana kuvamia makazi ya wafugaji wa jamii hiyo ya kisukuma kutokona na madai ya wakulima kushindwa kuvumilia kuonewa na baadhi ya tabia ya wafugaji wa kisukuma kulisha mifugo katika mashamba yenye mazao na pindi wanaporibu kuwaondoa mifugo hiyo 



huambulia kupigo na kupata majeraha na ulemavu. 




Baada ya msafara huo uliokuwa na kikosi cha askari wa jeshi la polisi saba nikiongozwa na Afisa wa Operesheni wilaya ya Morogoro Nicolaus Hekwe ulifanya kikao cha dhalula na viongozi wa serikali ya kijiji hicho kabla ya kulielekea katika makazi ya wafugaji watatu ambao wanadai kuwa ndiyo chanzo kikuu cha mgogolo huo kutokana na kulisha mazao katika mashamba ya wakulima huku kundi kubwa la vijana wenye silaha za jadi lifikiwa nyuma yao na usafiri wa pikipiki, baiskeli na wengine kutembea kwa miguu kuelekea kitongoji cha Lukoni. 




Msafara huo ulianza kufika katika makazi ya mfugaji moja Bangili Mwanabahati na kumkukuta mama mzazi na watoto watano huku mwenyewe akiwa ametoweka na mkewe pamoja na mifugo na kuelekea katika makazi ya Lutovisha Mwanapawa na Mguu wa Simba Mwanahingu ambako nako hawakufanikisha kukuta mtu kwenye makazi hayo. 




Wakati huo huo msafara wa kundi la wananchi wenye silaha za jadi lilikuwa tayari limefika katika makazi ya Bangili Mwanabahati baada ya kupata taarifa za kumkosa mmoja wa watuhumiwa wa mgogolo huo wananchi hao walichukuwa jukumu la kuchoma moto nyumba nne na kuanza kukamata kuku na kubeba vyombo vya ndani kabla ya kufanya vurugu hizo. 




Kutokana na kuwa na kundi kubwa la vijana walitumia uwingi huo kuwazidi maarifa askari hao na pamoja na mbunge kuendeleza kuchoma moto nyumba katika makazi ya Ndilana Ikilisha kwa kuchoma nyumba tatu ambapo zoezi hilo lilidumu kwa musa wa masaa mawili kabla ya kufanikiwa kurudisha kundi hilo kijijini hap. 




Mwandishi wa gazeti hili alifanya mahojiano na mama mzazi wa mfugaji wa jamii ya kisukuma Bangili Mwanabahati, Bi Njile Subii (70) juu ya kupata ukweli wa tukio hilo la madai ya wakulima kuhusu mwanae kulisha mifugo katika mashamba ya wakulima, kuwapiga na kuwajeruhi ambapo alisema yeye amekuwa akipata malalakio mengi juu ya vitendo hivyo na kumkanya mwanawe asiendelee na tabia hiyo lakini amekuwa mkaidi. 




Bi Subii alisema kuwa mwanae wakati mwingi anakuwa yupo malishoni na mifugo lakini yeye amekuwa akikumbana na malalamiko juu ya vitendo anavyofanya mwanae lakini amekuwa akimkanya bila ya mafanikio. 




Wakati huo huo Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Mwambungu alisema serikali haina tatizo na wafugaji wa jamii yeyote isipokuwa ina tatizo na wafugaji ambao wanashindwa kuafuata sheria zilizowekwa na serikali ya kijiji au serikali kuu na kuwa wanaoshindwa kuafuata sheria zilizowekwa watachukuliwa hatua za kisheria kama waharifu. 




Mwambungu alisema wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhala kuwa baada ya mgogolo huo kutokea analazimika kuunda tume huru ya watu watano itakayo kuwa na jukumu la kuhakiki upya idadi ya wafugaji walioingia katika kijiji hicho kihalali na wataobainika kuingia kinyume na sheria za kijiji hicho wataondolewa katika wilaya hiyo na kurudi walikotoka. 




Alisema kuwa ardhi haiiongezeki ila binadamu na mifugo imekuwa ikiongozeka kila mwaka hivyo kutokana na uwingi wa mifugo katika kijiji hicho ipo haja kuwaondoa wafugaji walioingia kiholela bila kuafuata taratibu hilo tutalishughulikia ili kuondoa kero hiyo ya wafugaji na wakulima na kumaliza kabisa mgogolo huo. 




Katika mgogolo huo umedumu kwa zaidi ya miaka miwili huku ikidaiwa baadhi ya wafugaji wa jamii ya kisukuma watatu Lutovisha Mwanapawa, Bangili Mwanabahati na Mguu wa Simba Mwanahingu wakidaiwa kuingia katika kijiji hicho bila ya kufuata taratibu za kisheria na wafugaji na kudaiwa kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima huku wakulima wakichukua jukumu la kuwaondoa au kuwakamata mifugo hiyo huambulia kipigo kinachosababisha kupata majeraha na kuvunjika viungo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...