Sunday 5 October 2014

RAIS KIKWETE ASHIRIKI SALA YA EID EL HAJJ UPANGA DAR ES SALAAM

D92A5402Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Hajj katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.(Picha na Freddy Maro)D92A5408D92A5531

Wednesday 1 October 2014

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA MAREKANI KWENYE MKUTANO WA 69 WA UMOJA WA MATAIFA

jk1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.

Sunday 28 September 2014

TBL YAFANIKISHA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA WIKI YA NENDA KWA USALAMA


 Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akikabidhiwa zawadi ya fulana  na Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo yenye ujumbe wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. katikati ni Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kulia ni kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika

PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE IN DIFFERENT ACTIVITIES IN NEW YORK

1

 President Jakaya Mrisho Kikwete greets Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 

PRESIDENT KIKWETE VISITS CNN STUDIOS IN NEW YORK ON SEPTEMBER 26, 2014

1

President Jakaya Mrisho Kikwete chats with  Cable News Network (CNN) ‘s Richard Quest and Maggie Lake when he visited  CNN Studios at the  Time Warner Cente in New York.  CNN is an American basic cable and satellite television channel that is owned by the Turner Broadcasting System division of Time Warner. The 24-hour cable news channel was founded in 1980 by American media proprietor Ted Turner.  Upon its launch, CNN was the first television channel to provide 24-hour news coverage, and was the first all-news television channel in the United States.While the news channel has numerous affiliates, CNN primarily broadcasts from its headquarters at the CNN Center in Atlanta, theTime Warner Center in New York City, and studios in Washington, D.C. and Los Angeles. CNN is sometimes referred to as CNN/U.S. to distinguish the American channel from its international sister network, CNN International.

Tuesday 9 September 2014

MBUNGE WA JIMBO MOROGORO KUSINI ATEKELEZA AHADI YAKE YA KUKUWEZESHA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOROGORO VIJIJINI

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris (kulia) Ahimkabidhi Pikipiki 11 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar Ikiwa Ni ahadi yake aliyoitoa ya Kukusaidia chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi.Mh Kalogeris Amekabidhi pikipiki hizo akiwa na Lengo Kila kata Kuwa na Pikipiki MMoja uwe Mradi wa Chama ili kuwezesha Kila kata Kuendesha Shuguli za Chama Bila kuwa wategemezi .Mbunge Kalogeris amehadi kuhakikisha kata zote za jimbo hilo zinapatiwa Pikipiki.Mh Kalogeris amesisitiza Pikipiki hizo ni mali ya CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini na si mali ya watu binafsi. 
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris  Akitoa hotuba yake Namna atakavyoshirikiana na Wanachama na Viongoizi wa Jimbo la Morogoro Kusini bega kwa bega ili chama hicho kiweze kujitegemea kiuchumi kwajili ya kutekeleza Majukumu yake ya Kila siku Ikiwemo Kushinda kwa kishindo Uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2O15.
Mwenyekiti wa CCM Morogoro Vijijini Mh Jazar akisisitiza jambo wakati akitoa neno la Shukrani mara Baada ya Kupokea Msaada ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini  Mh Kalogeris aaliyoitoa kwajili ya kukifanya Chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi.

Monday 1 September 2014

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA MOROGORO, AFANYA MAJUMUISHO NA WATENDAJI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris  alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Gairo ya kwenye kikao cha majumuisho na watendaji wa mkoa huo baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa wa Morogoro
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla

Wednesday 27 August 2014

MAELFU YA WANANCHI WAMLAKI RAIS KIKWETE GAIRO, KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

 : Rais Kikwete akihutubia umati wa maelfu ya wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014

Tuesday 26 August 2014

JK ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MZUMBE

1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro baada ya kuwahutubia chuoni hapo Agosti 25, 2014.
2
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika Chuo Kikuuu cha Mzumbe Morogoro baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha mzumbe ambapo walihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

RAIS KIKWETE AZINDUA BARABARA YA DUMILA-RUDEWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami. 

Monday 25 August 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI MJINI MOROGORO, AWATAKA VIONGOZI WAACHE WOGA KUSIMAMIA SHERIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania
(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi 
mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na
Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI MJINI MOROGORO, AWATAKA VIONGOZI WAACHE WOGA KUSIMAMIA SHERIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania
(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi 
mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na
Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014

Saturday 23 August 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE UZINDUA JENGO JIPYA LA SACCOS

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akikata  utepe  kuzindua jengo jipya la Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha kijiji cha Kinole, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014. Wengine ni Mama Salma Kikwete (kulia),  Mbunge wa Viti Maalum Dkt Lucy Nkya (wa [ili kulia) na Mwenyekiti wa SACCOS ya Kinole Mzee Issa Ramadhani Kambi

RAIS KIKWETE ATAWAZWA KUWA CHIFU MSAIDIZI WA WALUGURU NA CHIFU KINGALU HUKO KINOLE, MOROGORO, APEWA JINA LA CHIDUKILA

 CHIFU wa Waluguru Kingalu
Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.  Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha “muibukaji”, kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

Friday 22 August 2014

RAIS KIKWETE ASAFIRI KWA TRENI YA TAZARA KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa huo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera, Mbunge wa Morogoro Kusini  Mhe Innocent Kalogeris na KAtibu wa Rais Bw. Prosper Mbena wakiongea ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki mkoani Morogoro.

RAIS KIKWETE AWEKA AFUNGUA KITUO CHA AFYA KIBAONI, MOROGORO VIJIJINI


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Wabunge Mhe Abdul Mketeme (kushoto) na Mhe Getrude Rwakatale (kulia) wakifunua pazia kwa pamoja kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.

Thursday 21 August 2014

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa furaha wakati akielekea ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (kushoto) na Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais)
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni  Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa  Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)

Saturday 26 July 2014

ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA MKEWA MBUNG WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI

 Mkuu wa mkoa akimpeleka Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh  Innocent Kalogeris  kupokea mwili wa mpendwa mke wake,kulia ni dada wa mbunge huyo.   

Monday 9 June 2014

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA MH MWIGULU NCHEMBA ATIKISA MOROGORO

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris  akisalimia Wananchi.Wakati wa kumkaribisha Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara na Naibu waziri wa Fedha Mh Mwiguli Nchemba Kwenye Mkutano Wa hadahara katika Viwanja vya Fire Manispaa ya Morogoro. Mwigulu Nchemba akizungumza na Wakazi wa Morogoro amesisitiza kuwa Huu ni wakati wa Kupigania Ajira kwa Vijana na sio Muda wa Kurumbana kuhusu Idadi ya Serikali

Monday 24 March 2014

RAIS KIKWETE HAJAINGILIA MCHAKATO WA KATIBA

jk5Na Magreth  Kinabo –Maelezo
Umoja wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba la Tanzania Kwanza   wasema kwamba   Mhe. hotuba ya Rais,Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi  wa Bunge Maalum   la Katiba  ,haikururuga wala kuingilia mchakato wa kupata Katiba Mpya ,bali  alitoa maoni na ushauri kama kiongozi wa nchi.
Aidha wajumbe hao wamesema Rais hakuingilia kanuni za bunge hilo zilizopitishwa, hakubadilisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na hakupiga kura kwenye vifungu vya Katiba.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti  wa wajumbe hao, Said Nkumba katika mkutano na waandishi habari uliofanyika kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa Bunge mjini Dodoma.
 Nkumba ambaye aliambatana na  baadhi ya  wajumbe wengine watano , ambapo alisema  hotuba  hiyo  imeweka wazi faida na hasara za mifumo yote ya Muungano  wa Tanzania kwa hoja ili Watanzania wawe nnnnnna fursa pana ya kutafakari na kuamua
“ Rais ametimiza kauli yake ya kushawishi kwa hoja na si kulazimisha,” alisema Nkumba.

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA KAMPENI KATA YA MBWEWE

1Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ridhiwani Kik wete katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya shule ya sekondari ya Changarika kata ya Mbwewe jimboni humo, Ridhiwani Kikwete alishiriki yeye mwenyewe kijenga shule hiyo wakati ya sekondari Changarika akiwa katibu wa uhamasishaji UVCCM taifa na amewaomba wananchi wa kata hiyo kumkopesha imani yao kwake na yeye atawalipa maendeleo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- CHALINZE)3Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Pongwe Kiona kata ya Mbwewe leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo.6mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Juma Pinto Mkurugenzi wa Jambo Concerption na William Malecela kulia.

Saturday 22 March 2014

HOTUBA YA JK,WAKATI WA KULIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA



Mheshimiwa Samuel Sitta, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba;Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar;Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarMheshimiwa Anne Semamba Makinda; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ; Mheshimiwa Rashid Othman Chande, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;Mheshimiwa Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar; Viongozi Wakuu Wastaafu; Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba; Waheshimiwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; Wageni waalikwa; Mabibi na Mabwana; Pongezi Nakushukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kunipa fursa ya kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge letu Maalum la Katiba katika siku hii muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu. Nimekuja kuwatakia heri na naungana na Watanzania wenzetu wote kuwaombea baraka za Mwenyezi Mungu, ili muweze kuifanya kazi yenu kwa utulivu, hekima, umakini mkubwa na kuimaliza kwa salama na kwa mafanikio yanayoyatarajiwa na Watanzania. Natoa pongezi nyingi kwako na kwa Makamu wako kwa kuchaguliwa kwenu kuongoza Bunge hili maalumu na la kihistoria. Ushindi mkubwa mliopata ni kielelezo tosha cha imani kubwa na matumaini waliyonayo Wajumbe wenzenu kwenu. Matumaini yao ndiyo matumaini ya Watanzania wote, kwamba mtaliongoza vizuri Bunge hili, ili liweze kutimiza kwa ufanisi mkubwa jukumu lake muhimu sana katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Mwenyekiti;Niruhusu pia niwapongeze kwa dhati Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa bahati ya aina yake waliyopata ya kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fursa hii hutokea mara chache sana katika historia ya nchi yo yote na watu wake. Mkifanikiwa kuipatia nchi yetu Katiba nzuri majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu, katika kumbukumbu za historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni matarajio ya Watanzania kuwa mtatunga Katiba itakayokubalika na wengi. Katiba inayotekelezeka.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...