Friday, 12 April 2013

DKT. SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA MCC IKULU,ZANZIBAR LEO,PIA AKUTANA NA Uongozi wa Wizara ya Uwezeshaji


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Millenium Challenge Cooperation(MCC) la Marekani Daniel Yohannes,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,akiwa na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati)akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Millenium Challenge Cooperation(MCC) la Marekani Daniel Yohannes,akiwa na ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt, walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika,katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Watendaji na maafisa wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,katika kikao cha Uongozi wa Wizara hiyo,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa katika mpangilio wa Rais, kuzungumzia utekelezaji wa kazi za kila Wizara.Picha na RamadhanOthman,Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...