Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Watoto Sophia Simba akipewa
maelezo na Bill Marwa kuhusiana na tovuti rasmi iliyotengenezwa maalumu
kwa ajili ya kupaza sauti ya mwanamke (www.sautiyamwanamke.org) baada ya
kuizinduwa kwenye uzinduzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake
unaofanyika Dodoma. Waliosimama kushoto kwa waziri ni Teresa Yates na
Hilda Mashauri viongozi wa mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO
Gender Coalition) waandaaji wa mdahalo huo.Tovuti hiyo itatumika kutoa
taarifa za kila siku za mdahalo na kuendelea kupaza sauti ya mwanamke
baada ya mdahalo kwa kuandika habari mbalimbali zinazohusu mwanamke.
Jambo jingine muhimu la kufahamu ni kwamba Mh Simba amezindua rasmi www.sautiyamwanamke.org kwa ajili ya kusaidia katika harakati za kupaza sauti ya Mwanamke.
Dr.
Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akimkaribisha mgeni rasmi Mhe.
Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na
Watoto kwa ajili ya kufungua rasmi mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake.
Mshiriki
kutoka Unguja akizungumza kwa niaba ya wanawake takribani 300
wanaoshiriki mdahalo wa kitaifa wa wanawake uliozinduliwa leo Dodoma na
Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na
Watoto.
Mwanahamisi
Salim, Meneja wa Kampeni, Ushawishi na Utekelezaji wa Haki za Kiuchumi
kutoka shirika la Oxfam akiendesha zoezi la ufunguzi wa Mdahalo wa
Kitaifa wa Wanawake unaofanyika katika ukumbi wa Chimwaga Mjini Dodoma.
Teresa
Yates, Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania akikabidhi zawadi kwa
Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na
Watoto na kwa Dr. Rose Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Baadhi
ya Wanawake wanaoshiriki Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake. Mdahalo wa
Kitaifa wa wanawake ni tukio linalofanyika kwa hisani ya mtandao wa
jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) kuanzia tarehe 10-14
April, 2013 mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment