Waziri
wa Fedha Dk. William Mgimwa wa kwanza kushoto akisaini mkataba wa
makubaliano ya mkopo wenye riba nafuu kwajili ya ujenzi wa barabara kwa
kiwango cha lami, kulia ni Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana.
Masaki Okada akitia saini pia makubaliano hayo.
Waziri
wa Fedha Dk. William Mgimwa akibadilishana hati za makubaliano ya
mkataba na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada, mkataba
huo utaiwezesha Tanzania kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa
barabara hizo kwa kiwango cha lami.Waziri
wa Fedha Dk. William Mgimwa akisisitiza jambo akiwa na Balozi wa Japani
nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada mara baada ya kukamilisha kwa
shughuli za utiliaji saini wa makubaliaono ya mkopo wa riba nafuu.
………………………………………………………..
Na. Benedict Liwenga na Frank John-MAELEZO-DAR ES SALAAM
Serikali
ya Tanzania imetiliana saini mkataba na JAPAN wa shilingi Bilioni 129.4
ambao mkopo wa masharti nafuu kupitia shirika lake la maendeleo JICA
kwa ajili ya kuendeleza sekta ya barabara nchini.
Fedha
hizo ni kwa ajili ya kutekeleza mradi wa barabara awamu ya pili kwa
kiwango cha lami itahusisha urefu wa kilomita 203 ambayo ni kutoka
Mtambaswala, Mangaka hadi Tunduru kwenye ukanda wa Mtwara barabara hii
ambayo inaunganisha kusini mwa Tanzania pamoja na Msumbiji, Malawi na
Zambia.
Sherehe
hizo za utiaji wa saini zimefanyika leo jijini Dar es salaam ambapo
Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa na Japan
iliwakilishwa na Balozi Masaki Okada.
Kwa
upande wa Waziri wa Fedha Dk. Mgimwa aliishukuru serikali ya Japan
mikopo yenye masharti nafuu kwa Tanzania ambayo imechangia kwa kiwango
kikubwa kukuza maendeleo katika sekta ya barabara na kuahidi kuwa awamu
ya pili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami itatekelezwa kwa
kuzingatia makubaliano.
“Napenda
kukuhakikishia kuwa, serikali ya Tanzania itasimamia kwa karibu miradi
yote miwili ya ujenzi wa barabara kwa ufanisi mkubwa”, Dk. Mgimwa
alisisitiza.
Kwa
upande wake Balozi wa Japan Masaki Okada amefurahishwa na uhusiano
mzuri uliopo kati ya nchi yake na Tanzania ambao umedumu kwa zaidi ya
miaka hamsini sasa ikiwa ni kielelezo cha ushirikiano mzuri baina ya
nchi zote mbili.
Naye
Mwakilishi mkuu wa JICA nchini Tanzania Yasunori Onishi alisema kuwa
sekta ya usafirishaji imekuwa moja ya maeneo muhimu katika ushirikiano
kwani yanachangia ukuaji wa uchumi, ambapo alibainisha kuwa Japan
kupitia JICA imeweka vipau mbele kusaidia sekta ya usafirishaji katika
maeneo matatu ambayo ni, Kuimarisha miundombinu ya barabara
zinazounganisha nchi nzima, pili kupunguza msongamano wa magari katika
majiji kama vile Dar es Salaam na tatu ni maendeleo ya barabara
vijijini.
No comments:
Post a Comment