President
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete signs a condolence book at British High
Commissioner’s Office in Dar es Salaam following the death of former
British Prime Minister Margareth Thatcher who died of stroke on Monday
at the age of 87.(Photo by Freddy Maro).
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatano, Aprili 10, 2013 ametia saini Kitabu cha Maombolezo cha
aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Margaret Thatcher ambaye
alifariki dunia Jumatatu wiki hii kwa ugonjwa wa kiharusi akiwa na umri
wa miaka 87.
Rais Kikwete ametia saini Kitabu hicho kwenye Ubalozi wa Uingereza katika Tanzania ulioko Jengo la Umoja mjini Dar es Salaam.
Rais
alikaribishwa kwenye Ubalozi huo na Balozi wa Uingereza katika Tanzania,
Mheshimiwa Bi. Dianna Melrose na wafanyakazi wengine wa ubalozi huo na
amekwenda moja kwa moja kutia saini kitabu hicho mara baada ya kuwasili
kwenye Ubalozi huo.
Mara
baada ya kumaliza kutia saini Kitabu hicho, Balozi Melrose
amemwambia: “Kwa niaba ya Serikali ya Uingereza na Watu wa Uingereza
nakushukuru sana Mheshimiwa Rais kwa heshima hii ya kuja kutia saini
Kitabu cha Maombolezo cha Mheshimiwa Margaret Thatcher. Waziri Mkuu wa
nchi yetu atafurahi kujua kuwa umepata muda wa kuja kuungana nasi katika
kuomboleza kifo hiki.”
Naye
Mheshimiwa Rais Kikwete amemjibu: “Kwa mara nyingine Mheshimiwa Balozi
nakupa wewe binafsi, Serikali na watu wa Uingereza pamoja na familia ya
Bi. Margaret Thatcher salamu zetu nyingi za rambirambi kufuatia msiba
huu. Bi.Thatcher alikuwa kiongozi mashuhuri. Alikuwa kiongozi mwenye
nguvu na msimamo na ndiyo maana anaheshimiwa na sisi sote.”
Bi.
Margaret Thatcher alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa miaka 11 kati ya
1979 na 1990. Alikuwa mwanamke wa kwanza na pekee mpaka sasa kushikilia
nafasi hiyo na ndiye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza kukaa madaraka kwa
muda mrefu zaidi kuliko waziri mkuu mwingine yoyote katika kipindi cha
miaka 150.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
10 Aprili, 2013
No comments:
Post a Comment