Thursday, 11 April 2013

MAFURIKO YAATHIRI MAKAZI 450 MOROGORO KUSINI


ZAIDI ya kaya 450 katika kata nne tofauti zimekumbwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa kunyesha ambapo imebomoa nyumba, kusomba mifugo ikiwemo na kuharibu heka 233 za mimea ya mazao aina mbalimbali baada ya mvua kubwa kunyesha April 5 mwaka huu katika wilaya ya Morogoro Vijijini.
Akizungumza na wananchi wakati wa ugawaji wa chakula kwa wazee wasiojiweza kata ya Selembala Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris alisema kuwa mpaka sasa kuna kata nne ambazo zimekumbwa na mafuriko ambapo kaya zaidi ya 450 zimeathirika kutokana na mafuriko hayo.
Kalogeris alisema kuwa kutokana na mvua hiyo kunyesha na kusababisha mafuriko kaya hayo wananchi wamepoteza mali mbalimbali ikiwemo chakula, mifugo na kuharibu mimea ya mazao aina mbalimbali katika kata hizo.
“Njia ya kuwanusuru wananchi hao ambao wamekumbwa na janga la mafuriko kwa sasa kunahitajika zaidi ya tani 70 ama 80 za chakula cha haraka kwa ajili ya kuwagawia wahanga hao ili kuwanusuru na janga la njaa pamoja na kupatiwa mbegu za muda mfupi ili kuweza kupanda katika mashamba yao”. Alisema Klaogeris.

Kalogeris alisema kuwa kwa upande wa mbegu za muda mfupi zenyewe zinahitaji tani 50 au 60 ili kuweza kupanda katika kipindi hiki cha mvua za mwisho ili kuweza kupata mavuno yatayosaidia katika msimu ujao wa kilimo.
Alitaja kata zilizokumbwa na mafuriko hayo kuwa ni pamoja na Kisaki,  Bwakila Chini, Mvuha Selembala huku wananchi wa kata ya Selembala wakiathirika zaidi na mafuriko hayo.

Alisema kuwa leo (jana) nimetoa taarifa katika kamati ya ulinzi na usalama juu ya uhitaji wa tani za chakula na mbegu kwa waathrika hao.
Kalogeris alisema kuwa tayari mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi ametoa maagizo kwa maafisa watendaji wa vijiji kufanya tathimini ya uharibu wa mali na mimea ili kuweza kupata idadi kamili ya uharifu uliotokana na mafuriko hayo.
Katika mafuriko hayo kata ambayo imeathirika zaidi ni kata ya Selembala ambapo jumla ya nyumba 77 zimeharibika na heka za mimea ya mahindi, uvuta 233 katika kitongoji cha Bwila Chini.
Mbunge huyo ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro alikabidhi unga kilo 450 katika vitongoji vitano kwa ajili ya wazee wasiojiweza 30 wa kijiji cha Bwila Juu kupitia kwa vitongoji vya Kibiro, Umoja, Songambele na Muhunzi ambao kila kitongoji wazee sita walipatiwa unga katika kata hiyo.
Mafuriko hayo yalitokea baada ya mvua kubwa kunyesha kwa masaa 24 ikianza majira ya saa 4 usiku April 5 mwaka huu na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo nyumba, mifugo,mimea ya mazao na kupelekea baadhi ya wahanga wa mafuriko hayo kushinda juu ya miti kwa muda wa masaa matatu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...