Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (mwenye tracksuti ya bluu),Waziri wa
Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala (wa tano
kulia) na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole
Sendeka,wakishiriki katika matembezi ya nusu kilomita ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 29 tangu kufariki kwa Waziri Mkuu wa
zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,yaliyofanyika leo huko Kijijini
kwao Monduli Juu,Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la Maua kwenye Kaburi
la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,aliefariki
miaka 29 iliyopita siku kama ya leo.
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni
na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la
Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Wake wa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Mume wao.
Mbunge wa Jimbo la Arusha,Mh.
Godbress Lema akishiriki mbio za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu
Edward Moringe Sokoine zilizofanyika kijijini kwake Monduni Juu,Mkoani
Arusha leo.
Baadhi ya vijana wa jamii ya
Kimasai wakikimbia mbio fupi za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu
Edward Moringe Sokoine,kijijini kwake Monduli Juu,Mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment