Naibu Kaibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi upande wa Zanzibar, ndugu Vuai Ally Vuai.
Naibu
Kaibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi upande wa Zanzibar, ndugu Vuai Ally
Vuai ameeleza kuwa upo umuhimu mkubwa wa kuendelea kudumisha muungano
ulioasisiwa na muasisi wa Serikali ya mapinduzi na Chama cha ASP
Marehemu Abeid Amani Karume.
Mheshimiwa
Vuai ameyaeleza hayo katika Kongamano la kumuenzi muasisi wa
Mapinduzi-marehemu Mzee Abeid Amani karume lililoandaliwa na Jumuiya ya
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) chini ya mwenyekiti wake
Ndugu Sadifah Juma, lililofanyika katika Ukumbi wa chuo cha Ufundi
Karume, Mbweni Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa Umoja
huo akiwemo Katibu Mkuu wa UVCCM, ndugu Martine Shigela, Makatibu wa
Idara za UVCCM na maafisa wengine wa Makao Makuu Bara na Zanzibar, na
wajumbe wengine 600 kutoka katika Mikoa mbalimbali ya Zanzibar, pamoja
na wawakilishi kutoka vyuo vikuu.
Katika
Nasaha zake na salamu za ufunguzi wa Kongamano hilo, Mheshimiwa Vuai
alifafanua umuhimu wa kuwaenzi waasisi wa muungano na kusema kuwa vijana
wana wajibu wa kutafakari na kujifunza kutokana na viongozi wao
waliopita, wajifunze ujasiri, uzalendo na kusimamia misingi ya umoja na
utaifa. Alisema kuwa Mapinduzi yalikuwa ni halali kwa kuwa Serikali
iliyopinduliwa ilikuwa ni Serikali chini ya Sultan ikinufaisha wachache,
hivyo Mapinduzi yalilenga kuleta utawala ulio huru wa watu wa Zanzibar,
yalilenga kutetea Uafrika yakiongozwa na mioyo ya kizalendo na nia ya
kuijenga Zanzibar na kunufaisha wengi katika wazanzibar wenyewe.
Alisisitiza
kuwa muungano una manufaa makubwa kwa wanzanzibar akitolea mifano ya
manufaa yanayopatikana katika sekta mbalimbali za kimaendeleo na kijamii
ambapo alianza kwa kutaja manufaa yanayopatikana katika sekta ya Elimu
ambapo alitaja kuwa kupitia muungano , wanafunzi takribani 1251 waliweza
kupatiwa mikopo ya elimu ya juu chini ya bodi ya mikopo ya wanafunzi
(HESLB) ikiwa ni wanafunzi si zaidi ya mia nane na sitini (860) ndio
ambao waliweza kupatiwa mikopo na Serikali ya Mapinduzi hii ni kulingana
na bajeti na uwezo wa Serikali ya mapinduzi.
Lakini
pia, Mheshimiwa Vuai alitaja fursa katika sekta ya afya, ambapo akasema
kuwa wagonjwa mbalimbali ambao wamekuwa na matatizo makubwa na
yanayohitajia utaalamu zaidi wamekuwa wakipelekwa katika Hospitali Kuu
ya rufaa ya Muhimbili kama walivyo watanzania wengine kwa gharama ya
chini sawa na watanzania wengine, na akasisitiza haya yanapatikana chini
ya kivuli cha muungano. Akaeleza pamoja na fursa hii kuwepo kwa fursa
nyingine za makazi, biashara n.k
Pamoja
na kufafanua juu ya faida na manufaa hayo Mheshimiwa vuai alisema kuwa
ni kweli kuwa zipo kero mbalimbali katika muungano, ambapo akasisitiza
kuwa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) imejadili na
kutoa fursa kwa kero hizo kujadiliwa na kutafutiwa ufumbuzi. Mheshimiwa
Vuai alisema kama tatizo ni kujiunga na OIC, NEC ya CCM imetoa fursa ya
kulijadli hilo na kuruhusiwa ikionekana inafaa, ama ikiwa kero ni mapato
ya Bandari, ama mafuta ama takwimu basi NEC imetoa fursa ya kuyajadili
haya na ikionekana inafaa yatolewe katika muungano, na pia kulibainisha
suala la mahusiano ya kimataifa na suala la Zanzibar kujiunga na Umoja
wa Visiwa Duniani.
Akasisitiza
kuwa vijana wasiwe tayari kufuata mawazo ya wapinga mapinduzi na
wapinga muungano kwani hao ni watu wanaotaka kurudisha ukoloni kwa
mlango wa nyuma, kwa kuwa wanapinga muungano bila ya kuwa na sababu za
msingi wala hoja.
“..wakiulizwa
kwanini hamtaki muungano hali ya kuwa imetolewa nafasi ya kujadili kero
na kasoro zilizopo katika muungano ili uwe bora zaidi na wenye manufaa
zaidi, wapinga muungano husema tu kuwa hatutaki muungano, lakini sisi
wanaotuita wahafidhina tunajua kuwa wao ni mawakala wa ukoloni na
wapinga mapinduzi..” alisema Mheshimiwa Vuai.
Pamoja
na kuelezea kwa kina suala la muungano, Mheshimiwa Vuai aliwakumbusha
Vijana juu wajibu na jukumu lao la kushiriki katika uchaguzi wa wajumbe
wa mabazara ya katiba na kutumia haki yao hiyo ya kidemokrasia.
Kongamano
hilo la siku moja lilimalizika saa 12: 15 jioni, ambapo mada mbalimbali
kama Mchango wa Marehemu Karume katika Ukombozi wa Zanzibar
iliyofikishwa na Ndugu Haji Machano Haji pamoja na mada ya Fursa za
Kielimu, Kiuchumi na Kijamii, zilizopatikana baada ya Mapinduzi Matukufu
ya January 12, 1964 iliyowasilishwa na Haroun Suleiman (MNEC) na Mada
ya Mwisho kuwasilishwa ikiwa ni DHANA YA MAPINDUZI YA JANUARY 12, 1964
na kwanini yalifanyika ikiwasilishwa na Ramadhan A. Ramadhani (MNEC).
No comments:
Post a Comment