Thursday, 11 April 2013

ANGALIA PICHA ZA MAFURIKO MOROGORO KUSINI

 Makazi ya mkazi wa kitongoji cha Bwila Chini kijiji cha Bwila Chini kata ya Selembala akiwa amesimama nje ya nyumba yako kukumbwa na mafuriko katika kata hiyo ambapo jumla ya kata nne za wilaya ya Morogoro Vijijini kukumbwa na mafuriko April 5 mwaka huu mkoani Morogoro. 

 Wakazi wa kijiji hicho wakiwa nje ya nyumba yao wamekaa wakati wakimsubiri mbunge wa jimbo hilo la Morogoro Kusini.

 Mkazi wa kijiji hicho cha Bwila Amina Omari akiwa nje ya nyumba yao juu baada ya kukumbwa na mafuriko.
 Wakazi wa kijiji cha Bwila Chini wakitembea kwenye maji baada ya maji hayo kutuwama katika barabara na mashamba yenye mimea ya mahindi.
 Muonekano wa nyumba iliyokumbwa na mafuriko hayo.
 Mmea wa mhindi ukiwa umeng'olewa na mafuriko yaliyosababisha na mvua kubwa iliyonyesha April 5 mwaka huu.
 Mimea ya mahindi ikiwa imelala chini baada ya mvua kunyesha iliyoambanata na upepo katika kijiji cha Dutumi.
 Sehemu ya wakazi wa Bwila Chini wakiwa eneo la nyumba yao ambayo ilibomoka kutokana na mafuriko hayo.
 Watoto wa kijiji cha Bwila Juu akiwa wamebeba kiroba cha unga baada ya mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeris kutoa msaada wa kilo 450 za unga wa mahindi kwa ajili ya kuwagawia wazee wasiojiweza katika kata ya Selembala.
 Wakazi wa Bwila Chini wakiwa nje ya nyumba yao huku maji yakiwa yamezingira.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...