Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akiagana na Naibu Mkuu wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel mara
baada ya kumalizika kwa maongezi baina yao yaliyofanyika hivi karibuni
ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ubalozi wa Ujerumani umemualika
waziri Dk. Mukangara kuhudhulia mkutano wa mawaziri wa michezo Duniani utakaofanyika mwezi wa tano mwaka huu nchini Ujerumani.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akiangalia barua ya mwaliko wa kuhudhulia mkutano wa mawaziri wa Michezo Duniani utakaofanyika mwezi wa tano mwaka huu nchini Ujerumani. Kulia ni Naibu Mkuu wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel ambaye alimtembelea waziri huyo ofisini kwake hivi karibuni kwajili ya kumpelekea barua ya mwaliko.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akisoma taarifa kuhusiana na mkutano wa mawaziri wa Michezo Duniani utakaofanyika mwezi wa tano mwaka huu nchini Ujerumani. Kulia ni Naibu
Mkuu wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel ambaye alimtembelea
waziri huyo ofisini kwake hivi karibuni kwajili ya kumpelekea barua ya
mwaliko.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
No comments:
Post a Comment