Mmoja wa wanachama wa chama cha CHADEMA akikabidhi kadi yake kwa Ndugu Kinana na baadae kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM,akiwa ni mwanachama mpya aliyejiunga na chama hicho.
Baadhi ya Wanchi wa eneo la Ifakara
Mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana alipozungumza
nao eneo la Stendi kuu ya mabasi ya Ifakara mjini,Ndugu Kinana alizungumza
mambo mengi ikiwemo namna ya kufanya utatuzi wa mambo ambayo yamekuwa
kero kwao,ikiwemo suala la Umeme,Kilimo na miundo mbinu,sambamba pia kuisaidia
miradi mbalimbali inayofanywa na vijana wa mji wa Ifakara ambao unakuwa kwa
kasi siku hadi siku.
Ndugu Kinana akikazia jambo wakati
alipokuwa akizungumza na baadhi ya Wanchi wa eneo la Ifakara Mjini,eneo la
Stendi kuu ya mabasi ya Ifakara mjini,wilayani Kilombero mkoani Morogoro.Ndugu
Kinana aliwasifu na kuwapongeza vijana wa mji wa Ifakara kwa kuonyesha uwezo
wao mkubwa kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea.Ndugu Kinana yumo
mkoani Morogoro kwa ziara ya siku kumi ya kuimarisha chama cha CCM sambamba na
kukagua miradii mbalimbali kwa ajili ya maendelo ya wananchi,
Ndugu Kinana akifafanua jambo alipokuwa
akizungumza na baadhi ya wanachama wa Ifakara mjini kwenye mkutano wao ndani
mapema jana.
Mkuu wa wilaya ya Kilombero,Bwa.Hassan
Masalla akifafanua jambo kuhusiana na tatizo la kukatika katika kwa umeme
mbele ya wakazi wa mji wa Ifakara mjini mapema jana,aidha Masalla aliwatoa hofu
wananchi wa eneo hilo la Ifakara mjini kuwa tatizo hilo ambalo limekuwa kero
kubwa kwa wananchi wa eneo hilo linashughulikiwa kwa nguvu zote na kuhakikisha
linatengamaa na kwisha kabisa,kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdurahman Kinana akimsikiliza kwa makini.
wanachama wakimsikiliza Ndugu Kinana alipozungumza nao kwenye mkutano wao ndani,Ifakara Mjini wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro,ambapo alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo na suala zima la kukiimarisha chama hicho.
akizindua moja shina la Wakaretwa wa
chama cha CCM kati ya mashina manne aliyoyazindua Ifakara mjini.
Baadhi ya wakazi wa Ifakara Mjini eneo
la Sokoni,wakimsikiliza Ndugu Kinana alipozungumza nao kwenye eneo la mradi wa
chama hicho.
No comments:
Post a Comment