Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia wadudu wa ugonjwa wa Maralia kwa kwa kutumia Mashine ya
Hadubini, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa pamoja wa Kimataifa wa Watafiti wanasayansi wa
Afrika, alioufungua jana jijini Arusha.
Makamu
wa Rais Dkt. Bilal,akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuuwa Mawasiliano wa
Kampuni ya Utafiti, Mafunzo na Huduma ya Ifakara Health Institute,
David Mbulumi, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika
mkutano huo jana.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akisikiliza maelezo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika Mkutano huo, jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilali,
akifungua rasmi Mkutano wa Pamoja wa Kimataifa wa Watafiti Wanasayasi
Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya
Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS) ya Afrika Kusini. Kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dkt. Mwele Malecela. Mkutano huo wa siku nne
unafanyika Jijini Arusha.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya Pamoja na
Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo
(kushoto) na Dkt Martha Lemnge, baada ya kuwakabidhi tuzo zao hizo
jana.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na
Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo
(kushoto) na Dkt Martha Lemnge, baada ya kuwakabidhi tuzo zao jana.
Kulia ni Mkurugenzi wa NIMR, Dkt. Mwele Malecela.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR), Dkt. Mwele Malecela akisoma hotuba yake.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali.
Badhi
ya Watafiti Wanasayansi kutoka Taasisi zaidi ya 35 barani Afrika
wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa NIMR wakati wa hotuba yake
ya ukaribisho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa
Afrika (SACIDS), Mark Rweyemamu akisoma risala yake wakati wa ufunguzi
wa Mkutano huo Jijini Arusha.
Viongozi wa NIMR na Watafiti mbalimbali wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa SACIDS.
Mkurugenzi wa OHCEA, Japhet Kilewo akitoa hotuba yake.
Meza kuu ikifuatilia kwa ukaribu Hotuba ya Mkurugenzi wa OHCEA.
Mwakilishi kutoka Umoja wa Afrika (AU)Dk. Ahmed Hamdy akizungumza na Wanasayansi watafiti.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid nae alisoma Hotuba
ya Wizara na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo.
Wakuu
wa Taasisi za kitaifa na Kimataifa pamoja na wanasayansi watafiti
wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
Makamu
wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, pamoja na Mkurugenzi wa NIMR, Dkt.
Mwele Malecela wakizindua rasmi awamu ya nne ya Vipaumbele vya Tafiti
za Afya kwa mwaka 2013-2018.
Pia Makamu wa Rais alipata fursa ya kuzindua Mpango wa Afya Moja nchini Tanzania.
Aidha
Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal, pia alizindua Mpango
wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS)
No comments:
Post a Comment