Viongozi wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiimba Wimbo wa Mataifa hayo kabla ya kuanza kwa Mkutano wao wa 11 kwenye Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha. Kutoka Kushoto kuelekea kulia ni Waziri Mkuu wa Rwanda Bw. Pierre Damien Habumuryemi, Rais wa Burundi Bw. Pierre Nkurunziza, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Uhuru Kenyata wa Kenya na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Sheni.
 Rais Uhuru Kenyata wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya akihutubia Mkutano wa Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza baada ya Kuchaguliwa kuwa rais wa Kenya hivi Karibuni.
 Baadhi ya Mawaziri wa SMT na SMZ walioshiriki Mkutano wa Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya Ngurdogo Mkoani Arusha Tanzania. Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais MBM Dkt. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Fatma Abdullhabib Fejeji, Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sita na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tanzania Mh. Mahadhi Juma.
Mwenyekiti wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Kaguta Museveni aliyeshika Kofia akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake wa jumuiya hiyo mara baada ya kumaliza Mkutano wao wa 11 wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ngurdoto Mkoani Arusha. Kushoto kwa Rais Museveni ni Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais Uhuru Kenyata wa Kenya na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Sheni. Kulia kwa Rais Museveni ni Waziri Mkuu wa Rwanda Bw. Pierre  Damien Habumuryemi pamoja na Rais wa Burundi Bw. Pierre Nkurunziza.