Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaasa Waheshimiwa Wabunge kutumia Lugha ya Kistaarabu kuchangia mijadala Bungeni.Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola, akiomba Mwongozo kwa Spika BungeniNaibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mhe. January Makamba akijibu baadhi ya hoja zilizochangiwa Bungeni leo.Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtembu akichangia Mjadala
Spika wa Bunge Anne Makinda amewaasa Wabunge kutumia Lugha ya Staha ambayo ni ya Kibunge wakati wa kuchangia mijadala Bungeni.
Mhe.
Makinda amesema, kuendelea kutumia lugha ya matusi, kejeli na maudhi
kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ni kuendelea kuliondolea hadhi Bunge.
Pamoja
na hilo, wabunge wanatakiwa kujikita katika kuchangia hoja zenye
kutataua matatizo ya wananchi ili kutimiza wajibu wa kila mbunge wa kuwa
wakilisha wananchi.
Mhe.
Makinda , amesema, fursa ya kila Mbunge kuchangia lazima ilenge kutatua
matatizo ya wananchi na sio kutukanana na kusahahu jukumu lilomblele ya
kila Mbunge.
Katika
Picha ni baadhi ya waheshimiwa Wabunge waliochangia mjadala wa
kupitisha Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2013/14 Mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment