Wednesday, 17 April 2013

MKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA BUNENGI YA AFRIKA KUSINI KWA URATIBU WA NDC AONANA NA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KWA LENGO LA KUSAIDIA KATIKA UWEKEZAJI MKOANI HUMO

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Bunengi ya Afrika Kusini Bi. Savannah Maziya akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NDC (National Development Coorporation) ambaye pia Mbunge Mstaafu wa Jimbo la KwelaNdugu Chrissant Mzindakaya walipoonana na uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kujadili namna Kampuni hiyo kwa kushirikiana na NDC katika uratibu watakavyosaidia katika kuwekeza kwenye miundombinu ya bandari, reli na barabara kuunganisha Mkoa wa Rukwa Mikoa pamoja na Nchi jirani kuwezesha rasilimali zilizopo Mkoani Rukwa zinapata masoko yakiwemo mazao, madini na utalii. Utalii huo ni pamoja na Kalambo Falls maporomoko ya maji makubwa barani Afika na Bismark Fort iliyokuwa ngome ya wajerumani iliyopo hapa Mkoani Rukwa.
 Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang’a akiongoza kikao hicho kilichohudhuriwa na muwekezaji huyo, wawakilishi wa NDC, Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa na Halmashauri za Wilaya ya Kalmbo na Sumbawanga.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta akiwa anazungumza katika kikao hicho.
 Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwa anatoa mchango wake juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa muwekezaji huyo.
Afisa katika dawati la Uwekezaji Ndugu Misasi Marco akimwaga sera kutoka katika dawati lake uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...