SERIKALI
ya Zanzibar , imesema inajiandaa kujenga nyumba za makaazi kwa ajili ya
askari wa Jeshi la Polisi, pamoja na vituo vya kufanyia kazi. Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed,
aliyasema hayo jan wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni
jaaku Hashim Ayoub, aliyetaka kujua kama serikali ina mpango wa kujenga
nyumba hizo katika ukanda wa utalii.
Akijibu
suala hilo Waziri huyo alisema ni kweli serikali inalazimika kuuona
umuhimu huo baada ya kuona sekta ya utalii ni muhimu kwa pato la taifa
na tayari imeanza kujenga nyumba hizo.
Alisema nyumba na
vituo vya kazi kwa ajili ya askari Polisi tayari mradi huo upo ambao
utekelezaji wake unafanywa kwa pamoja na wafadhili, mbali mbali kwa
kushirikiana na wananchi.
Aidha, Waziri huyo
alisema katika kuutekeleza mpango huo, hivi sasa wameweza kujenga kituo
cha Polisi cha Nungwi, Kiwengwa na Paje ikiwa pamoja na kukamilisha
ujenzi wa nyumba ya makaazi katika eneo hilo la Paje.
Alisema kazi hiyo
inaendelea kufanyika katika kuyaangalia maeneo mengine ya ukanda wa
utalii ili kuweza kujenga nyumba hizo mpango ambao unaenda sambamaba na
kuimrisha ulinzi wa Polisi jamii.
Hata hivyo Waziri
huyo, alisema katika kukabiliana ana hali hiyo, pia serikali katika
ukanda huo, imeweza kuunda kikosi kazi cha ulinzi kwa ajili ya maeneo ya
utalii kutokan ukanda wa pwani ya Mashariki biashara hiyo imeimarika.
Kuna mabadiliko
yameanza kufanyika anakamilisha mfumo wa Baraza la Manispaa kwani
likiyumba kidogo linaweza kusababisha kutokea kwa matatizo.
Serikali imeunda jopo la mawakili
kupitia ripoti ya Kamati teule ya Baraza la Wawakilishi juu ya utendaji
wa Baraza la manispaa ili kuona namna ya kulifanyia kazi ambapo hapo
baadaea litafikishwa BLM Mawakili ambapo alisema imo katika hatua za
mwisho kusajili wageni
No comments:
Post a Comment