Tuesday, 16 April 2013

RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI NCHINI UHOLANZI

8E9U4742Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Serikali ya Uholanzi ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje wan chi hiyo Bwana Frans Timmermans jijini The Hague Uholanzi. 8E9U4762 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi. 8E9U4773Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi. 8E9U4949Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha mbegu bora za mazao ya mboga ya Rijk Zwaan  Bwana Kees Reinink akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baadhi ya miche inayotokana na mbegu bora wakati Rais alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague,nchini Uholanzi jana. Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SAGCOT Bwana Geoffrey Kirenga.Kampuni ya RIJK ZWAAN tayari imewekeza nchini Tanzania huko Arusha ambapo inazalisha mbegu bora za mazo ya mbogamboga zilizofanyiwa utafiti kudhibiti magonjwa. 8E9U5077Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Utafiti na Uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga ya RIJK ZWAAN jana katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague. 8E9U5354 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na Malkia Beatrix wa Uholanzi wakati walipomtembelea Malkia huyo katika makazi yake Rasmi jijini The Hague jana.Rais Kikwete yupo nchi Uholanzi kwa Ziara rasmi.Picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...