Monday, 15 April 2013
TASWIRA ZAIDI CCM WANAVYOTIKISA MOROGORO KWA SASA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Luaha Kilosa Mkoani Morogoro wakati yeye akiongozana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati katibu mkuu huyo alipofanya ziara katika eneo hilo, Katibu mkuu huyo yuko katika ziara ya kikazi ya kuhimiza maendeleo na kukagua miradi ya maendeleo ili kuisimamia serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwahamasiha wananchi katika kushiriki shughuli za maendeleo
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa Luaha Kilosa mkoani Mrogoro
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM akisalimiana na wananchi mbalimbali waliofika kumlaki wakati alipowasili kijijini hapo
Wananchi wakiserebeka na muziki kabla ya kuanza kwa safari hiyo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na Mohamed Seif Khatib Mjumbe wa NEC Oganizesheni na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Luaha Kilosa
Ndugu Mohamed Seif Khatib akizungumza na wananchi wa Luaha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment