L Mwenyekiti wa Kata na wenzake 68 watimkia CCM
Wadai Chadema imekubuhu kwa utapeli
Wadai Chadema imekubuhu kwa utapeli
NA BASHIR NKOROMO, GAIRO
TSUNAMI ya ziara ya Katibu Mkuu wa
CCM, mkoani Morogoro imeiacha CHADEMA taaban wilayani Gairo baada ya
Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Mkalama wilayani hapa, Zefania Magiga
na wenzake 68 kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara, jana,
Aprili 18, 2013.
Magiga na wenzake walikabidhi kadi
zao za Chadema kwa Kinana, na kupewa kadi za CCM, baada ya kutangaza
kukihama chama chao na kujiunga na CCM kwenye mkutano huo ambao
ulifurika mamia ya wananchi, kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Gairo B,
katika wilaya mpya ya Gairo.
Mbali na kupokea wanachama hao
kutoka Chadema, kwenye mkutano huo, Kinana alipokea wanachama wapya 120,
waliojunga na CCM na kufanya jumla ya wanachama wapya waliojinga na CCM
kwenye mkutano huo kuwa 188.
“Ndugu wana Gairo wenzangu na Watanzania wote, mimi kwa nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Kata, nilikuwa naongoza wanachama wengi wa Chadema, na nilikuwa si mtu mdogo, lakini kwa muda ambao nimekuwa ndani ya chama hicho nimebaini kuwa viongozi wake wa kitaifa ni matapeli wa hali ya juu, ndiyo maana mimi na wenzangu tumeamua kuhamia CCM”, alisema Magiga. Alisema, akiwa Chadema alikuwa akishangaa kuona kwamba kila agizo alilokuwa akipokea kutoka viongozi hao wa chama hicho lilikuwa na kumwagiza kushawishi wananchi shari na kukataa kutii sheria za nchi, jambo ambalo alisema kwa muda mrefu akikuwa hakubaliano nalo kwa kuwa ni tofauti na lengo lililokuwa limemwingiza Chadema tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 15 iliyopita.
“Kwa kuwa sasa nnimeamua kurejea rasmi CCM, na hawa wenzangu (67) nimewaelimisha kwamba Chadema ni chama hatari nao wakanielewa sasa leo tunahamia wote CCM tunaomba mtupokee bila kinyongo, maana kufanya kosa si kosa kosa ni kulirudia”, alisema Magiga baada ya kukabidhiwa kadi yake ya CCM na Kinana. Akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, alisema, uoamuzi wa wananchi wanaojiunga na CCM sasa na hata baadaye ni wa busara sana kwa sababu CCM ndicho chama ambacho bado cha kuaminika kwa malengo na matarajio yote ya maendeleo, amani na usalama wa Watanzania. Kinana aliwataka wananchi wa Gairo na Tanzania kwa jumla kuendelea kuiunga mkono CCM ili iendelee kuwatumikia kwa kuwa bado ni chama imara kutokana na kuasisiwa katika misingi ya uhakika. Mapema kabla ya mkutano huo, Kinana alifika katika kata mbalimbali wilayani Gairo na kufungua mashina ya Wajasiriamali wakereketwa wa CCM, ambapo pamoja na kuyafungua aliwahimiza kushina hayo kama kicocheo cha kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa lengo la kukuza uchumi wao na wa taifa. “Tunapofungua mashina haya hatukusudii kuwa vijiwe vya kupigia soga tu, bali tunawataka wanachama wetu wa CCM myatumie kukaa pamoja na kuunda vikundi vya ushirika na kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ambazo zinawatoa kwenye kulalamika kwamba hakuna ajira kwa kuwa mtakuwa tayari mnazo shughuli za kufanya”, alisema Kinana. Kinana alifungua zaidi ya mashina saba, abayo aliawaahidi wanachama wake kuwapa ushirikiano mkubwa katika kuwasaidia kuinuka kiuchumi ambapo baadhi aliahidi kuwapa fedha au vitendea kazi kwa ajili ya kuanzisha au kuendeleza shughuli zao za maendeleo.
No comments:
Post a Comment