Sherehe za AU zinafanyika huku Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto pamoja na mtangazaji wa redio Joshua Arap wakiwa za ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007/08 katika mahakama ya kimataifa ya ICC.
Duru zinasema kuwa huenda mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Afrika wamekubaliana kuhusu azimio linalotaka kesi ya washukiwa hao kurejeshwa Kenya ambako inaweza kusikilizwa na hatua kuchukuliwa dhidi ya watakaopatwa na makosa.
Shereha hizi pia zinakuja wakati bara la Afrika linashuhudia migogoro nchini Mali, DRCongo huku Misri ikiwa bado haijatengamaa baada ya kufanyika mapinduzi ya kiraia yaliyomng'oa mamlakani rais Hosni Mubarak.
Lakini mwenyekiti wa AU ana matumaini kuwa Afrika iko kwenye mkondo mzuri wa kimaendeleo.
Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 21 wa AU, Dlamini Zuma alisema kuwa Afrika imekuwa kiuchumi katika muongo mmoja uliopita, imeshuhudia maendeleo ya kiuchumi , ustawi wa kikanda , uimarishwaji wa miundo mbinu na ushirikiano wa kikanda.
Sherehe hizi ambazo zitafuatwa na mkutano wa siku mbili wa marais wa AU, zitatoa fursa kwa wananchi wa bara la Afrika kuangazia ufanisi wa Muungano huo.
No comments:
Post a Comment