
Baadhi ya Viongozi, Wajumbe na Wanachama Wapya katika picha ya pamoja

Mwenyekiti wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Maina Ang’iela Owino akimkabidhi vitendea kazi ikiwemo katiba ya chama kwa Ndugu Chande Kigwalilo mwenye kofia Mwenyekiti Shina jipya la Cardiff.

Katibu wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Bi. Mariam Mungula akimkadhi kadi za wanachama wapya Katibu wa shina Jipya la CCM Cardiff Bi. Rosemary Kiputa.

Mwenyekiti wa TAWI LA CCM UK Ndugu Maina Ang’iela Owino akiongoza nyimbo za chama katika shamrashamra za ufunguzi wa shina jipya la CCM CARDIFF WALES.

Wajumbe wakitega sikio kusikia machache toka kwa Mwenyekiti wa TAWI LA CCM UK
Ndugu Maina Owino hayupo pichani.

Naibu Katibu CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Albert Ntemi, Naibu katibu Itikadi Siasa na Uenezi CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Abraham Sangiwa na Bi Rose Kiputa Katibu shina jipya la Cardiff wakifuatila kwa makini mada muhimu katika ufunguzi huo.

Mwenyekiti wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Maina Ang’iela Owino akimkabidhi vitendea kazi ikiwemo katiba ya chama kwa Ndugu Chande Kigwalilo mwenye kofia Mwenyekiti Shina jipya la Cardiff.

Katibu wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Bi. Mariam Mungula akimkadhi kadi za wanachama wapya Katibu wa shina Jipya la CCM Cardiff Bi. Rosemary Kiputa.

Mwenyekiti wa TAWI LA CCM UK Ndugu Maina Ang’iela Owino akiongoza nyimbo za chama katika shamrashamra za ufunguzi wa shina jipya la CCM CARDIFF WALES.

Wajumbe wakitega sikio kusikia machache toka kwa Mwenyekiti wa TAWI LA CCM UK
Ndugu Maina Owino hayupo pichani.

Naibu Katibu CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Albert Ntemi, Naibu katibu Itikadi Siasa na Uenezi CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Abraham Sangiwa na Bi Rose Kiputa Katibu shina jipya la Cardiff wakifuatila kwa makini mada muhimu katika ufunguzi huo.

Makamu Mwenyekiti CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Said Sukwa akitoa yake machache katika ufunguzi huo.

Wajumbe wa Shina jipya la CCM Cardiff Wales.

Wajumbe na wanachama wapya CCM Shina la Cardiff.

Naibu Katibu Itikadi Siasa na
Uenezi CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Abraham Sangiwa katika picha ya
pamoja na Mwenyekiti wa Shina la CCM Cardiff Ndugu Chande Kigwalilo na
Mjumbe wa Shina la CCM Cardiff Bi. Prudencia Kimiti.

Viongozi waliochaguliwa Shina la
CCM Cardiff wakichukua nafasi zao aliyesimama na kutoa machache ni Ndugu
Chande Kigwalilo Mwenyekiti Shina la CCM Cardiff akiwashukuru wajumbe
kwa kumpa nafasi ya kuongoza shina hilo.

Wajumbe wa CCM Cardiff wakipeana mkono wa pongezi toka kwa Mwenyekiti CCM UK Ndugu Maina Owino.

Dr. Abdallah Saleh Mwenyekiti wa CCM Shina la Northmpton akifafanua jambo katika ufunguzi huo.

Bi. Prudencia Kimiti Mjumbe wa CCM
Shina la Cardiff akitoa shukrani zake kwa uongozi wa TAWI LA UNITED
KINGDOM kwa kuwezesha ufunguzi wa Shina Jijini CARDIFF.
Katika
ufunguzi huo Jumamosi tarehe 11 Mei 2013 ulijaa shamrashamra na nderemo
na kuhudhuriwa na viongozi wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi
la CCM UNITED KINGDOM Ndg Maina Ang'iela Owino, Makamu Mwenyekiti
Ndugu Said Sukwa, Katibu Bi. Mariam Mungula, Naibu Katibu Ndugu Albert
Ntemi, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Leybab Mdegela, Naibu
Katibu Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Abraham Sangiwa, Katibu wa Uchumi
na Fedha Ndugu John Juma Lyimo, Naibu Katibu Uchumi na Fedha Ndugu
Mohamed Upete na wanaCCM toka mashina mbalimbali ya CCM UK.
Mwenyekiti
wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM Ndg Maina Ang'iela Owino aliwashukuru
Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni
na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Ndg Owino aliwakumbusha kuwa
uhalali wa shina lao unajumuishwa katika Sera ya nje na matawi yake
katika Katiba ya CCM.
Ndg Owino
aliwakumbusha kuwa kujiunga na CCM kunaambatana na kuzingatia masharti
ya kuheshimu watu, kufanya juhudi za kuielewa, kuielezea, kuitetea na
kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM. Pia kwamba CCM inathamini haki na
wajibu wa mwanachama.
Aidha Ndg
Owino hakusita kuwakumbusha kuwa CCM na Serikali yake inaendelea
kujijenga na kuboresha taasisi zake ili kuendana na mahitaji ya kizazi
na wakati uliopo na hivyo basi wanaCCM Cardiff wasioneane haya wala
kuogopa kuchagua viongozi wenye sifa za kutosheka na wasio tawaliwa na
tamaa na watakao zingatia miiko ya uongozi kama inavyoainishwa katika
katiba ya CCM.
Kabla ya
kuhitimisha hotuba yake Ndg Owino alichambua na kuainisha kwa kina na
kuishirikisha halaiki kufanya tathmini ya wazi ya jinsi CCM imeiongoza
serikali kutekeleza ilani yake ya uchaguzi ya 2005/2010 na mafanikio
dhahiri yanayopatika katika kutatua kero za wananchi. Aidha alisema
baadhi ya changamoto zilizopo nchini ni matokeo ya mabadiliko endelevu,
kukua na kuendelea kwa mifumo na taasisi za umma na sekta binafsi na
kwamba CCM na serikali yake inaendele kujiimarisha kuyakabili kwa
mikakati na mipango endelevu ya muda mfupi na mrefu, pia Ndugu Maina
aliwakumbusha Wana CCM UK Kuwa mchango wao unathaminiwa na ni wamuhimu
katika kuleta mabadiliko yatayowanufaisha wengi katika nyanja mbalimbali
muhimu za kimaendeleo na kichumi
Idara ya
Itikadi Siasa na Uenezi na ile ya Uchumi na Fedha walitoa machache
yanayohusu idara zao na namna zinavyofanya kazi ili kuwapa mwanga
wanachama wapya na viongozi katika shina hilo.
Ufunguzi huo ulifuatiwa na uchaguzi wa Viongozi mashina uliosimamiwa na Katibu wa CCM UK, Bi Mariam Mungula.
Viongozi waliochaguliwa katika shina hilo jipya la Cardiff – Wales ni;
- 1. Chande Kigwalilo Mwenyekiti wa Shina
- 2. Bi. Rosemary Kiputa Katibu wa Shina
- 3. Prudencia Kimiti Mjumbe wa Shina
- 4. Munde Nyirambo Mjumbe wa Shina
- 5. Alen Mguto Mjumbe wa Shina
Mara
baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa shina jipya la Cardiff Ndugu Chande
Kigwalilo alitoa machache na kushukuru wajumbe na wanachama kumpa nafasi
ya kuliongoza shina na kushukuru uongozi wa tawi kwa kufanikisha
ufunguzi huo na kuwakarakibisha Jijini Cardiff.
Imetolewa na Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi
CCM TAWI LA UNITED KINGDOM
No comments:
Post a Comment