Mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa na waziri katika ofisi ya rais sera na mahusiano, Mh.Steven Wasira (kushoto) akiteta jambo na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi,Hassan Tati wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM katika uchaguzi wa udiwani kata ya Iseke.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM wilaya ya Ikungi, Jonathan Njau (wa kwanza kushoto) akifuatilia kwa makini maendeleo ya uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi wa nafasi ya udiwani kata ya Iseke.Wa pili kushoto ni MNEC wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Lawrence Masha, mbunge wa jimbo la Kibaha, Mudi Ijumaa na mbunge wa jimbo la Tarime mkoani Musoma, Nyagwana Nyambiri.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa na waziri katika ofisi ya rais sera na mahusiano, Mh. Steven Wasira (kushoto) akikabidhiwa kadi 350 za CHADEMA na aliyekuwa katibu kata wa chama hicho kikubwa cha upinzani, Francis Antoni.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa na waziri katika ofisi ya rais sera na mahusiano, Mh. Steven Wasira akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za nafasi ya udiwani kata ya Iseke wilaya ya Ikungi.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM na waziri katika ofisi ya rais sera na mahusiano, Mh. Steven Wasira (kushoto) akimnadi mgombea wa CCM Amosi Mughenyi anayewania nafasi ya udiwani kata ya Iseke.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa na waziri katika ofisi ya rais sera na mahusiano, Mh. Steven Wasira,akizindua tawi la CCM kijiji cha Unyangwe.
MNEC (CCM) wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jonathan Njau (mwenye shati kijani) akishiriki kikamilifu kutoa burudani na kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Unywagwe kwenye mkutano wa kampeni za kuwania udiwani kata ya Iseke.(Picha na Nathaniel Limu).







No comments:
Post a Comment