Saturday, 15 June 2013

MAMA SALMA APOKEA TUZO YA MILENIUM DEVELOPMENT GOALS, WOMEN’S PROGRESS AWARD 2013

IMG_7012Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Millenium Development Goals, Women Progress Awards,2013, kutoka kwa Ms Jennie Yeung , Rais wa Shirika la Sun Zhong Shan Foundation lililo chini ya United Nations Education, Science, Cultural and Health Advancement  Foundation la nchini Marekani.  Mama Salma alipokea tuzo hiyo baada ya kutimiza baadhi ya malengo ya Millenia katika masuala ya ukimwi, elimu kwa watoto waliokosa fursa  na kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini Tanzania. Kulia ni Katibu wa WAMA, Ndugu Daud Nassib na kushoto ni Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.PICHA NA JOHN LUKUWI – MAELEZO
IMG_6806Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Mali Mrs Mintou Doucoure  Epse Traore wakati walipohudhuria sherehe ya kupokea tuzo ya Millenium Development Goals 2013, Women Progress Award inayotolewa na Shirika la Voices of African Mother’s la nchini Marekani. Sherehe hiyo ilifanyika huko New York kwenye jengo la Umoja wa Mataifa tarehe 13.6.2013IMG_6809Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Denise Nkurunziza, Mke wa Rais wa Burundi wakati wa sherehe za kupokea tuzo zilizofanyika huko New York nchini Marekani tarehe 13.6.2013.IMG_6838IMG_6846Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Equatorial Guinea, Mama Dona Constancia Mangue de Obiang wakati wa hafla ya kupokea tuzo ya Millenium Development  Goals, Women Progress Award  2013 inayotolewa na Shirika la Voices of African Mother’s  la nchini Marekani tarehe 13.6.2013.
IMG_7119Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana rasmi na Mwanzilishi na Rais wa Voices of African Mother’s  Inc  Mrs Nana- Fosu Randall, ambaye shirika lake ndilo lililotoa tuzo kwa wake wa Marais wa Afrika waliotimiza baadhi ya malengo ya millennia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...