Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Christine Ngonyani akiwa na watumishi wa wizara ya fedha akifafanua kuhusu mikopo inayotolewa na wizara ya fedha.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Bw. William Ghump akifafanua jambo kuhusu Mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha.
Mkuu wa Serikali Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Wizara ya Fedha Bi. Christine Ngonyani akifafanua jambo kwa wananchi wa Ghana.
Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma akijibu swali kutoka kwa Mwanajeshi wa Ghana aliyekuwa anataka kujua ni jinsi gani Wizara ya fedha inawasaidia wanajeshi ambao wanataka kujikwamua kiuchumi.Wakushoto kwake ni Bw. Midladjy Maez(Mkatamiti) ambaye ni Maneja wa Mahusiano TRL akisikiliza kwa makini maelezo hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Bi Christine Ngonyani akiwa na Miriam Mnzava kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Ingiahedi Mduma wakiwapatia huduma wakuu wa jeshi la Magereza la nchini Ghana.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Christine Ngonyani akimpatia vipeperushi Bw. S.M Gyepi- Garbrah Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Ofisi ya Rais wa Ghana wakati wa Maadhimisho ya maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Nchini Ghana.


No comments:
Post a Comment