KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi baada ya kufungua tawi la CCM la Kitongoji cha Wangamiko, Kata ya Malangali wilaya ya Wanging’ombe, Machi 31, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji ilani ya Chama, na pia kukagua na kuimarisha uhai wa Chama katika mkoa wa Njombe. (Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Njombe leo Juni 1, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga. (Picha na Bashir Nkoromo).
Na Bashir Nkoromo – Njombe.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, amesema ziara yake mkoani Njombe imempa imani kwamba CCM itaendelea kuaminiwa na wananchi kwa muda wa miaka mingi ijayo kuiongoza Tanzania.
Amesema imani hiyo ameipata baada ya kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa huo na kushuhudia mwitikio mkubwa wa wananchi katika kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi, hadi katika maeneo ya vijijini ambayo ni magumu kufikika.
Katika ziara hiyo ambayo anafuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Kinana ametembelea wilaya za Makete, Wanging’ombe, Ludewa, na Njombe.
Kinana amesema, changamoto iliyobakia kwa viongozi wa CCM ni kuwatembelea wananchi wa kawaida bila kujali kuwa ni wana CCM wenzao, ili kuzungumza na kusikiliza kero zao kwa lengo la kuzifanyia kazi, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi inakamilika kwa kiwango kilichotarajiwa.
Amesema, ili kuendeleza imani waliyonayo wananchi kwa CCM, ni lazima viongozi wa Chama na wale wa serikali, wajenge tabia ya kuwaeleza wananchi kinagaubaga kuhusu mafanikio au changamoto zinapojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo au huduma za kijamii.


No comments:
Post a Comment