Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) akimsikiliza kwa makini Balozi wa Uholanzi nchini, Dk Ad Koekkoek (kushoto) wakati walipokuwa wanajadiliana masuala mbalimbali. Balozi huyo ambaye hivi karibuni anamaliza kipindi chake cha miaka minne ya kuwa balozi nchini ameishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ushirikiano wake. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. Balozi wa Uholanzi nchini, Dk Ad Koekkoek (kushoto) akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, mara baada ya kumaliza majadiliano yao yalikuwa yakifanyika ofisini kwa Mhe. Dk Nchimbi jijini Dar es Salaam. Balozi huyo ambaye hivi karibuni anamaliza kipindi chake cha miaka minne ya kuwa balozi nchini ameishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ushirikiano wake. Picha zote na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
No comments:
Post a Comment