NA JENNIFER CHAMILA NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuweza katika mkoa wa Tabora kwa kutumia rasilimali zilizopo katika sekta mbalimbali mkoani humo.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Makamu wa Rais Dk. Bilal wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji la Mkoa wa Tabora liliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam,ambalo limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo wawekezaji, wadau wa maendeleo, wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo.
Makamu wa Rais , Dk. Bilal aliwataka wawekezaji hao kuwekeza kwa kutumia rasilimali ambazo ni asali, madini,maeneo ya kihistoria, ujenzi wa hoteli,sehemu za kupumzika, viwanja vya michezo gofu, usafiri nchi kavu na angani,ufugaji wa wanyama wa porini,kampuni za kitalii, uwindaji wa wanyama, vivutio vya kiutalii vya kiutamaduni na kihistoria.
“Serikali inawahamasisha wawekezaji wa sekta binafsi na wawekezaji ambao watashirikiana na Serikali katika maeneo hayo,” alisema Dk. Bilal.
Dk. Aliongeza kuwa milango iko wazi kwa uwekezaji wa miundombuni ambayo, barabara kubwa, madaraja, mwasiliano ya simu, viwanja vya ndege, usambazaji miundombinu ya maji, hivyo wawekezaji kutoka nje ya nchi wanaruhusiwa kuwa umiliki wa zaidi ya asilimia 100 mipango ya kuhamisha na ujenzi inaruhusiwa kupitia maeneo hayo.
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Fatma Mwassa alisema wahahitaji shirikiano wa uwekezaji huo na kukuza masoko na tayari wameshaandaa mazingira mazuri.
“Ardhi tunayo tumeshaipima,tunahitaji wawekezaji katika kilimo, mafuta , nyama, maziwa na madini,” alisema Fatma.
Naye Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta alisema mkoa huo umepata kiongozi mzuri na watendaji na umejipanga ipasavyo juu ya jambo hilo.
“Kuanzia sasa mtumishi anapimwa kwa matokeo ya kazi yake . Tusiwe tunalalamika sisi ni masikini tutumie fursa zilizopo ili kuondoa umaskini kinachotakiwa ni uongozi usimamizi bora ili kuondokana na umaskini,” alisema Waziri Sitta.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC), Julieth Kairuki alisema taasisi hiyo imejipanga vizuri ili kusaidia uwekezaji katika mkoa huo na itaweka vituo mbalimbali.
Aliongeza kuwa hivi sasa kunawawekezaji 36 waliojitokeza kuwekeza kabla ya kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment