Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(Vazi la Kitenge)akiangalia Samani mbalimbali za Majumbani ambazo zinapatikana katika Banda la Jeshi la Magereza zilizotengenezwa kwa ubunifu mkubwa na Wafungwa kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Magereza( aliyepo kushoto) ni Mkuu wa Banda la Maonesho la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Julius Sang'udi akimuonyesha Kamishna Jenerali Samani hizo zilizopo katika Banda la Magereza.
--
Na Inspekta Lucas Mboje, Jeshi la Magereza
Jeshi la Magereza Nchini limeibuka Mshindi wa Pili katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa kwa upande wa Samani za Majumbani(Home Furnitures) ambapo Mshindi wa Kwanza ni Jeshi la Kujenga Taifa na Mshindi wa Tatu ni Funiture Centre ya Jijini Dar es Salaam.
Jeshi la Magereza Nchini limeibuka Mshindi wa Pili katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa kwa upande wa Samani za Majumbani(Home Furnitures) ambapo Mshindi wa Kwanza ni Jeshi la Kujenga Taifa na Mshindi wa Tatu ni Funiture Centre ya Jijini Dar es Salaam.
Hafla ya Kutangazwa Washindi Walioshiriki Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa imefanyika leo katika Ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa uliopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Awali, Mhe. Waziri Mkuu kabla ya kukabidhi Zawadi kwa Washindi Walioshiriki Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa alizundua Rasmi Nembo ya Zao la Asali ya Tanzania na "Bar Codes" itakayotumika kutambulisha Asali ya Tanzania Kimataifa.
Katika hotuba yake kwa Wananchi wa Tanzania, Mhe. Waziri Mkuu amewataka kujivunia na kuitumia ipasavyo fursa hii ya zao la Asali katika Biashara Kimataifa ambapo ametolea mfano wa kuigwa na hata kwenda mbele zaidi ya Nchi ya Ethiopia ambayo ni ya kwanza kwa Afrika na ya Nne Kimataifa katika kuzalisha na kuuza Asali katika Masoko ya Kimataifa.
Aidha ameyashukru Makampuni mbalimbali ya Ndani na Nje ya Nchi pamoja na Wananchi mbalimbali ambao wamejitokeza kikamilifu kushiriki katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa na amewataka Watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuinua Uchumi wa Mtanzania Mmoja Mmoja na wa Taifa kwa Ujumla.
Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea yalizunduliwa Rasmi na Mfalme Mswati wa III wa Swaziland tarehe 1 Julai, 2012 katika Ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa uliopo Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment