Saturday, 27 July 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA VIKUNDI VYA MTANDAO WA WAKULIMA WA TANZANIA (MVUWATA) MJINI MOROGORO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Picha na OMR
  Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro. Picha na OMR
 Wakulima wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa Tanzania (MVUWATA) wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa maandamano leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo, yaliyopokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi. Picha na OMR


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...