Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Rais wa Sri Lanka Mheshimiwa Mahinda Rajapaksa wakati wa mkutano wa smart partnership dialogue 2013 unaofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar es Salaam kuanzia tarehe 28.6.2013.Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mfalme Mswati wa Swaziland na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Benard Membe wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais Kikwete kwa Marais na wajumbe wa mkutano wa smart partnership unaofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 28.6 hadi 30.6.2013.Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akijiandaa kuzungumza na wake wa Marais na Wakuu wa nchi wakati wa mkutano wa smart partnership tarehe 29.6.2013 kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar es Salaam. Baadhi ya wake wa viongozi mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa smart partnership wakimsikiliza Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye ukumbi wa Mwalimu Nerere tarehe 29.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mke wa Mfalme wa Mswati wa Swaziland, Inkhosikati Lambikiza (kushoto), na Mwakilishi wa Mke wa Rais Joseph Kabila wa DR Congo (kulia) wakimwalika Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia Mama Charlotte Scott (hayupo pichani) kujiunga nao katika picha ya pamoja mara baada ya kikao chao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 29.6.2013.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi wanaohudhuria mkutano wa smart partnership unaofanyika hapa Dar es Salaam. Kutoka kushoto no Mama Charlotte Scott, Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia akifuatiwa Inkhosikati Lambikiza, Mke wa King Mswati, Mama Salma Kikwete, akifuatiwa na Mama Siti Hasma, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Malasya Mahathir Mohammed na kulia ni mwakilishi wa Mke wa Rais wa DR Congo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mama Siti Hasma mara baada ya kuhudhuria kikao cha wake wa marais na wakuu wa nchi kwenye mkutano wa smart partnership.Mke wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na Inkhosikati Lambikiza wa Swaziland.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mama Charlotte ScottMama Salma Kikwete na Inkhosikati Lambizana wakijiandaa kwenda katika chakula cha usiku kilichoandaliwa kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mfalme Mswati wa Swaziland mara baada ya chakula cha usiku.Rais Jakaya Kikwete akiiagana na Waziri Mkuu wa Malasya Mheshimiwa Najib Razak mara baada ya viongozi hao kupata chakula cha usiku kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere tarehe 29.6.2013.
PICHA NA JOHN LUKUW
No comments:
Post a Comment