Thursday, 25 July 2013

MATUKIO YALIYOJIRI KATIKA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MASHUJAA MOROGORO

Muonekano wa eneo la Mnara wa mashujaa uliopo eneo la Posta wakati wa maadhimisho ya sherehe ya kuwakumbuka mashujaa waliopoteza maisha katika vita kuu ya pili ya dunia na zile za Kagera mwaka 1978/1979 iliyoadhimishwa kimkoa eneo hilo la posta mkoani Morogoro leo julai 25/ 2013.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera  akipokea heshima muda mfupi kabla ya kuanza sherehe za kuwakumbuka mashujaa kwa mkoa wa Morogoro.
  
Haya ndiyo majina ya waliopoteza maisha.
 Mwakilishi wa Shekhe Mkuu wa mkoa wa Morogoro Ustadh Ally Said akiomba dua.
 Kiongozi wa dhehebu la Ahamaddiya naye akiwaombea dua njema askari hao waliofariki dunia katika vita wakati wa maadhimisho ya mashujaa.
Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoriki jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude akiwaombea dua njema askari waliofariki dunia wakati wa vita katika kilele cha mashujaa.
Kaimu Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Morogoro, George Pindu akisoma kwa kunukuu moja ya kifungu kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia katika maadhimisho hayo.


 Hiki ni kikosi cha maombezi kikitoa heshima zao za mwisho wakati wa kilele cha maadhimisho hayo.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro Anthony Mtaka wa pili kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali katika sherehe hizo.
 
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera aliyejishika mikono akiwa na viongozo mbalimbali wakati wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...