Meya wa jiji la Arusha amefyatuka na kuwataka wanasiasa kuwapelekea wananchi maendeleo na kuachana na kauli za kumuondoa meya huyo na malumbano yasiyo na tija kwa wakazi wa jiji la Arusha kwani utaratibu wa kanuni na sheria zipo wazi na hazihitaj malumbano kwakuwa yupo kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha Meya huyo Gaudency Lyimo alikuwa akijibu swali aliloulizwa kumekuwepo na malumbano ya muda mrefu kiasi cha kupachikwa majina kuwa meya wa kichina huku wanasiasa wakijinadi kuwa ataondoka kwenye kiti hicho baada ya uchaguzi mdogo uliopita mjadala wa meya hauna tija kwa wakazi wa jiji hilo.
Meya Lyimo amesema kuwa wakati huu si wa kulumbana bali ni wakati wa kuwaletea wananchi maendeleo kwani siku hazirudi nyuma na wanaofikiri mawazo hayo wanakosea kwani kila nchi inasheria na kanuni walizojiwekea na hata halmshauri inaongozwa kwa mujibu wa sheria hivyo suala hilo lipo kisheria .
Lyimo amewataka wanasiasa wanaopita kuhoji uhalali wa meya huyo kuwa ataondoka wana ndoto za mchana kwani yeye yupo kisheria na kanuni zinazoendesha halmashauri hapa nchini huku akiwataka madiwani waliochaguliwa kuweka mbele maslahi ya wakazi wa jiji na kuwaletea maendeleo.
Malumbano hayo yalianzishwa baada ya uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye jimbo la Arusha kwa chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA)kudai kuwa muda wa meya huyo unahesabika kwani idadi yao au koramu inatosha kumuondoa meya huyo.
Huku vyombo mbali mbali vya habari vikiripoti kuwa meya akalia kuti kavu ndipo waandishi walipoamua kumhoji meya huyo kupata msimamo wake kwenye suala hilo.
No comments:
Post a Comment