Saturday, 20 July 2013

MWENGE WA UHURU WALAKIWA KWA SHANGWE MKOANI RUKWA LEO UKITOKEA MKOANI KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na viongozi wengine pamoja na watumishi wa serikali ya Mkoa huo wakishangilia mapokezi ya mwenge wa uhuru uliowasili Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 19 Julai 2013, ukitokea Mkoani Katavi. Ujumbe wa mwenge mwaka huu ni “Tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini, itikadi, rangi na rasilimali”. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na viongozi wengine pamoja na watumishi wa serikali ya Mkoa huo wakishangilia mapokezi ya mwenge wa uhuru uliowasili Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 19 Julai 2013, ukitokea Mkoani Katavi. 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya mapema leo tarehe 19 Julai 2013, baada ya mwenge huo kumaliza ziara yake Mkoani Katavi na kuanza ziara ya siku nne Mkoani Rukwa. 
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Juma Ali Simai akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Challa B leo tarehe 19 Julai 2013. Mwenge wa Uhuru umeanza ziara yake ya siku nne Mkoani Rukwa kwa kuanzia na Wilaya ya Nkasi na kuendelea Kalambo na Sumbawanga. 
Baadhi ya watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifurahia mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...