Mhe. Membe na Mhe. Al Sabah wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu Ushirikiano katika masuala ya Siasa kati ya Tanzania na Kuwait. Tukio hilo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2013. Kulia ni Bw. Benedict Msuya, Afisa Mambo ya Nje.
Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Al Sabah (hayupo pichani) walipokutana. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (wa kwanza kushoto kwa Mhe. Membe), Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Prof. Abillah Omar (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto)
Mhe. Al Sabah akizungumza na Mhe. Membe (hayupo pichani).
Mhe. Al Sabah akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mhe. Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimkaribisha nchini Mhe. Sheikh Khalifa Al Hamad Al Sabah, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Membe akimpatia maelekezo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Naimi Aziz ambaye alishiriki mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Al Sabah.
Mhe. Prof. Omar (katikati) na Balozi Yahya (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kutoka kushoto ni Bw. Abas Mngwali, Bw. Hassan Mwamweta na Bi. Tagie Daisy Mwakawago.Picha na Ally Kondo.
No comments:
Post a Comment