Mlezi wa CCM mkoa wa Iringa waziri mkuu Mizengo Pinda (kushoto ) mkewe Tunu Pinda wakiweka shada la maua katika kaburi la diwani Iddi Chonanga leo
Picha na habari na Francis Godwin Blog- Mzee wa matukio Daima
WAZIRI mkuu Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa leo ameongoza wakazi wa mkoa wa Iringa katika mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli marehemu Iddi Rashid Chonanga huku akijitolewa kusomesha watoto wake wawili na yatima mmoja aliyekuwa akisomeshwa na marehemu Chonanga.
Waziri Pinda alitoa ahadi leo katika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa wakati akitoa salam zake za rambi rambi kwa wakazi wa kata ya Nduli na wananchi wa mkoa wa Iringa kufuatia kifo cha diwani huyo .
Alisema kuwa kifo cha diwani Chonanga kimeacha pendo ndani ya familia na hata katika chama chake cha CCM kutokana na mchango mkubwa ambao amepata kuutoa katika kupigania chama hicho na kuwa kutokana na maombi kusomeshwa yaliyotolewa na watoto hao ambao waliyatoa jana alipofika kuhani msiba huo katika kijiji cha Nduli
Kuwa kwa upande wake amejitolea kuisaidia familia hiyo
ya Chonanga kwa kusomesha mtoto mmoja anayeendelea na masomo katika chuo cha IFM jijini Dar es Salaam pia kumsomesha kijana wake mmoja ambae yupo sekondari pamoja na kuendelea kumsomesha mtoto mmoja yatima ambae diwani Chonanga alikuwa akimsomesha katika shule ya Sekondari ya Miyomboni mjini Iringa.

Mbali ya kujitolea kusomesha watoto hao bado waziri Pinda alilitaka baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kumuenzi diwani Chonanga kwa kazi kubwa za maendeleo alizozifanya katika kata yake kwa kuisaidia
familia yake .
familia yake .
“ Mimi nawashauri madiwani pamoja na mkurugenzi wa Manispaa kutokana na mchango mkubwa ambao diwani Chonanga aliutoa katika kuwatumikia wananchi wa kata ya Nduli ….sasa kuangalia uwezekano wa kuisaidia familia yake…..sisi kama chama leo tulikuwa na Halmashauri kuu ya CCM tumechangishana kiasi cha zaidi ya Tsh 800,000 ambazo tunazikabidhi kwa familia”
Katika hatua nyingine waziri Pinda amekipongeza chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini chini ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa katika mazishi hayo .
“ Kweli kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kuwashukuru sana viongozi wa Chadema Iringa chini ya mbunge mchungaji Msigwa kwa ushiriki mzuri wa mazishi ya diwani Chonanga ….nasema ahsanteni sana mheshimu mbunge Msigwa na wananchi wote ambao leo mmefika hapa”
Awali akiendesha ibada ya mazishi hayo msaidizi wa askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Blaston Tuluwene Gavile alitaka viongozi wa serikali na kisiasa kukumbuka kumcha Mungu na kuiga mfano wa Chonanga ambae mbali ya kufanya shughuli za kisiasa ila katika dini alikuwa mstari wa mbele akiwa kama mshauri wa usharika wa
Nduli .
Nduli .
Alisema kuwa mara kwa mara Chonanga alikuwa akipigania maendeleo ya
kata yake ya Nduli na wananchi wake na kuna wakati alipata kumtamkia wazi wazi kuwa yupo tayari kufa na hata agopa binadamu yeyote katika kuwapigania wananchi wake.
kata yake ya Nduli na wananchi wake na kuna wakati alipata kumtamkia wazi wazi kuwa yupo tayari kufa na hata agopa binadamu yeyote katika kuwapigania wananchi wake.
“ Marehemu alikuwa mtetezi wa kweli wa maendeleo ya wananchi wake
ndani ya chama chake na hata katika kanisa pia ndio maana leo umati mkubwa wa watu wamejitokeza kumzika ila sisi kama kanisa tunasema kifo katika Kristo ni furaha kubwa na leo hii mama mzazi wa Chonanga ambae ana miaka zaidi ya 83 ameomba kubatizwa rasmi “

Akisoma histori ya marehemu Chonanga mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo alisema kuwa Chonanga alizaliwa mwezi Februari ,1947 katika kijiji cha Malolo wilaya ya Kilosa na elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya kati ( Middle School ) Kidodi wilaya ya Kilolo na kujiunga na mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Songea mkoani
Ruvuma mwaka 1970
Ruvuma mwaka 1970
Katika uhai wake marehemu aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi mwaka 1972 ambapo miongoni mwa shule alizopata kufundisha ni pamoja na Mwembetogwa ,Kilimani , Nyabula, Nduli na Kitelewasi zilizopo mkoani Iringa pia marehemu aliwahi kuwa mratibu elimu kata ya kalenga kuanzia mwaka 1994-1999 alipostaafu kwa mujibu wa sheria na mwaka 2000 alifanya kazi ya ualimu kwa mkataba wa mwaka mmoja
Katika uongozi amepata kuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Nduli kati ya mwaka 2000-2005 na mwaka 2010 alichaguliwa kuwa diwani wa kata ya Nduli katika Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Iringa na katika baraza la madiwani
wa Halmashauri hiyo alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya maadili na mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi .
wa Halmashauri hiyo alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya maadili na mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi .
Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake alikuwa ni
jasiri ,mfuatiliaji wa mambo,mshauri na mjenga hoja katika vikao vya madiwai .
jasiri ,mfuatiliaji wa mambo,mshauri na mjenga hoja katika vikao vya madiwai .
Marehemu Chonanga alianza kusumbuliwa na maradhi
ya moyo usiku wa tarehe 2/7/2013 na alfajiri ya tarehe 3/7/2013
alipelekwa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kupata matibabu na mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari ila zilishindikana na majira ya saa 7;45 mchana alifariki dunia .marehemu Chonanga ameacha mjane mmoja watoto 10 na wajukuu 9

Mungu ailaze roho ya marehemu Iddi Rashid
Chonanga mahali pema peponi
Chonanga mahali pema peponi
AMINA
No comments:
Post a Comment