Thursday, 12 September 2013

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE SHINYANGA VIJIJINI

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakishiriki katika ujenzi wa Birika la Kunyweshea mifugo linalojengwa katika Kata ya Didia Jimbo la Solwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani Shinyanga, ambapo leo katibu Mkuu huyo ameendelea na ziara yake ya siku nne mkoani humo na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuimarisha uhai wa chama hicho na utekelezaji wa Ilani ya ya Uchaguzi.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE -SHINYANGA. 1 
 2 
Hili ndilo soko la Didia 16 
Wapiga ngoma wa Kikundi cha ngoma cha Didia wakipiga ngoma wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa soko la Didia. 18 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliomsimamisha katika kijiji cha Mwabenda ambao walikuwa na mabango yaliyokuwa yakielezea kero zao katika kijiji hicho ambazo zilikuwa ni Umeme na maji hata hivyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ndugu Ally Rufunga aliwaelezea mipango ya serikali kuhusu kijiji hicho katika kuhakikisha maji na umeme vinapatikana mapema katika kijiji hicho. 19 
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Salawe katika jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. 21 
Mama na mwana wakahudhuria katika mkutano huo. 25 
MNEC Azza Hilal Hamad kutoka Viti Maalum mkoa wa Shinyanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kijijini Salawe. 27 
Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akiwahutubia wapiga kura wake katika kijiji cha Salawe ambapo mkutano wa hadhara umefanyika leo. 28 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...