Wednesday, 9 October 2013

MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VILIVYOPIGANIA UHURU BARANI AFRIKA WATEMBELEA KAMBI YA IHEMI-IRINGA

1aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akiowaonyesha Makatibu Wakuu wa Vyama vilivyopigania uhuru wa nchi zao barani Afrika na ujumbe wa chama cha Kikomunisti cha China CPC huku wakiwa wamesimama kwenye jiwe kubwa linaloweza kuonyesha eneo hilo vizuri zaidi, Kulia ni Billy Masetlha Mjumbe wa Kamati kuu na Mahusiano wa Chama cha  ANC Cha Afrika Kusini .2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akiowaonyesha Makatibu Wakuu wa Vyama vilivyopigania uhuru wa nchi zao barani Afrika na ujumbe wa chama cha Kikomunisti cha China CPC wakiangalia ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli nje kidogo ya Manispaa ya  Iringa.
3Baadhi ya majengo mabweni madogomadogo yanavyoonekana kwa juu eneo lenyewe linavyoonekana6Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribisha wageni wake mara baada ya kufika katika kambi ya Ihemi mkoani Iringa leo kutoka kulia ni Obed Papela kutoka ANC na Naibu Waziri ,Didymas Mutasa Katibu MKuu wa chama cha ZANU- PF cha Zimbabwe, kutoka kushoto ni Dino Matrose Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA cha Angola na mwenye shati jeupe ni Filipe Paunde Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO cha Mozambique na mkalimani wake.8Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimuonyesha eneo hilo Ai Ping aliyevaa kofia Naibu Waziri wa mambo ya Nje wa China kutoka chama cha Kikomunisti cha China CPC ukubwa wa eneo hilo.11Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Billy Masetlha Mjumbe wa Kamati kuu na Mahusiano wa  Chama cha  ANC Cha Afrika Kusini  katika kijiji cha Ihemi mahali ambapo kitajengwa chuo hicho.12Viongozi hao wakilitazama eneo hilo kwa upande wa pili wa barabara kuu ya Iringa- Mbeya- Tunduma.14Kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Asha Rose Migiro na Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Chrstine Ishengoma pamoja na wageni wengine wakiwa katika ukumbi wa mkutano Kambi ya Ihemi.15Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM kulia akisalimiana na Lucas Kisasa aliyewahi kuwa mhariri Mkuu wa Uhuru Publication.16Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM akionyesha eneo hilo kwa upande wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya.17Wakiendelea kutathmaini eneo hilo.18Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Emanuel Mteming’ombe akiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa vijana wa mkoa wa Iringa Ahmed Asas.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...