
Mhe. Mwigulu Nchemba akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa tawi la CCM Columbus, Ohio siku ya Jumamosi Sept 28, 2013.
Wanachama wa tawi katika picha ya pamoja na Mhe. Mwigulu Nchemba mara baada ya kukata utepe.
Wananchama wa CCM Columbus wakionyesha kadi za chama hicho baada ya Mhe. Mwigulu Nchemba kufungua tawi siku ya Jumamosi Sept 28, 2013 mjini humo.
Mhe. Mwiugulu Nchemba akiongea na wanachama hao wa tawi la CCM Columbus, Ohio mara tu alipofanya uzinduzi.
Baada ya uzinduzi wageni wahemimiwa na wenyeji wao wakiburudika na vimiminika na kubadilishana mawili matatu.Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ( Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara) ameendelea kuwa na mafanikio katika ziara yake ya ki-chama Marekani.
Jumamosi iliyopita (i.e. September 28th, 2013) Mh. Mwigulu alifungua tawi la CCM Jimbo la Ohio kwa mafanikio makubwa kabisa.Kwa niaba ya chama, Uongozi wa tawi la Ohio unatoa Shukrani za dhati kwa watu wote waliohudhuria ufunguzi wa tawi na baadae mkutano wa maswali na majibu
No comments:
Post a Comment