Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipunga mkono Kwa Wanannchi wakati akivuka kwa mtumbwi kwenye Mto Ruhuhu ambao ni mpaka wa Wilaya za Ludewa na Nyasa katika mikoa ya Njombe na Ruvuma wakati alipotembelea kivuko cha mto huo ambacho kinafanya kazi kwa miezi minne tu kwa sababu ya kina cha maji kuwa kifupi wakati wa kiangazi, Serikali imeamua kujenga daraja katika mto huo lakini pia itajenga bwawa la mitambo ya kufua umeme wenye megawati 200 na pia mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika wilaya za Ludewa na Nyasa. Kinana amemaliza ziara yake katika mkoa wa Ruvuma na kesho atapanda meli pamoja na ujumbe wake kuelekea Kyela katika mkoa wa Mbeya tayari kwa ziara ya mkoa huo , Kinana yuko katika ziara ya mikoa mitatu ya Ruvuma, Mbeya na Njombe akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho huku akihimiza uhai wa chama cha mapinduzi CCM, kulia anayepunga mkono ni Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-LITUHI-NYASA).Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa akiwa katika picha picha ya pamoja na maofisa wa usalama kutoka jeshi la polisi.Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akifurahia jambo wakati alipokuwa akivuka mto Ruhuhu kwa kutumia mtumbwi anayepunga mkono ni Said Makala Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Televisheni cha Chanel Ten.Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi kushoto na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa wakiwa katika picha ya pamoja kandokando ya mto Ruhuhu mpakani mwa mikoa ya Ruvuma na Njombe Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizung8mza na wananchi wa Lituhi katika mkutano uliofanyika kwenye shule ya msingi ya Lituhi. Kivuko cha MV Ruhuhu kikionekana kwa mabli katika picha, kivuko hicho hakina kazi kwa sasa kutokana na kina kifupi chama maji watu wanavuka kwa kutumia mitumbwi.Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa akisalimia wananchi katika kijiji cha Kipingu Wilayani Ludewa leo.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa wakiwapungia mikono wananchi wakati wakivuka mto Ruhuhu kwa mtumbwi.Kivuko cha mto Ruhuhu kikiwa kimeegeshwa kandokando ya mto huo.Mtoto ambaye hakufahamika jina lake akipia ngoma wakati kikundi chan ngoma kikitumbiza katika mapokezi ya katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka mto Ruhuhu Mpakani mwa wilaya ya Nyasa na Ludewa.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana aksalimiana na wananchi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa leo wakati alipotembelea na kukagua miradi ya mto Ruhuhu.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na mkuu wa wilaya ya Ludewa juma Solomon Madaha wakati alipotembelea na kukagua miradi ya mto Ruhuhu leoKikundi cha ngoma kikipiga Mganda laini katika kinini cha Mkiri wilayani Nyasa leo wakati Abdulrahman Kinana alipokagua mradi wa ujenzi wa nyumba mbili katika zahanati hiyo zinazojengwa na taasisi ya Mkapa Foundation.Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi na mzee Mathias Ngwale Mwenyekiti wa tawi la MkiniKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipaka rangi moja ya nyumba za watumishoi wa wizara ya afya katika zahanati ya kata ya Mkiri wilayani Nyasa leo, anayeangalia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kapteni John Komba Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi akizunguza na wananchi katika kata ya Mkini wakati alipokagua zahanati hiyo kulia ni Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye shule ya msingi Lituhi mjini Lituhi.Wananchi wa jimbo la Mbinga Magharibi wakichukua mabati yao waliyopewa na mbunge huyo kupitia kampeni ya Jenga nyumba upate bati iliyoanzishwa na Kapteni John Komba mbunge wa jimbo la Mbinga Magharini.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wanalituhi leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule ya msingi ya Lituhi mahali ambapo mbunge huyo alizaliwa na kusoma hapo.
No comments:
Post a Comment