DAR ES SALAAM NOVEMBER 11, 2013.
Aidha, katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka (1976 – 1977), mwendesha mashtaka wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, 1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo cha polisi Dar es salaam, (1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Magomeni na Kinondoni na Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam (1987 – 1993),
Pia, amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Arusha, ( 1993 – 1995), Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi ( 1995 – 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi, (1996 – 1997), Mkuu wa kitengo cha usalama wa nchi, intelijensia na madawa ya kulevya makao makuu ya upelelezi (1997 – 2001) na kuwa msaidizi wa mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (2001 – 2006). Kuanzia mwaka 2006 hadi anastaafu, alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini.
Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, amemshukuru na kumpongeza (DCI) Manumba anayestaafu kwa kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi kwa weledi na uwaminifu mkubwa wakati wote alipokuwa mtumishi ndani ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:-
Advera Senso – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment