Msafara wa mkuu wa wilaya ya Morogoro na mbunge wa jimbo la Morogoro kusini wakiangalia uchafu uliorundikana juu ya daraja la
mto Dutumi baada ya kusimbwa na mafuriko yalitokea usiku wa April 5 mwaka huu na kuharibu makazi ya wananchi katika kata za Mvuha, Bwakila Chini, Mngazi na Kisaki ikiwemo na mimea ya mazao mbalimbali kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro.
Tope likiwa limejaa juu ya daraja la mto Mvuha baada ya mafuriko yalitokea usiku wa April 5 mwaka huu na kuharibu makazi ya wananchi katika kata za Mvuha, Bwakila Chini, Mngazi na Kisaki ikiwemo na mimea ya mazao mbalimbali kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro.
Wakazi wa kata ya Mvuha wakipita katika barabara yenye maji ya mafuriko ambayo hutumiwa na magari yatokayo Dar es Salaam kuingia wilaya ya Morogoro Vijijini kufuatia mvua kubwa kunyesha.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
WAKULIMA wa zao la mpunga zaidi ya 40 katika kitongoji cha Matunya kilichopo katika kijiji cha Dutumi walilazimika kupata juu ya miti ili kujiokoa na kifo baada ya kitongoji hicho kukumbwa na mafuriko April 6 mwaka huu wilaya ya Morogoro vijijini.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika kijiji cha Dutumi Mwenyekiti wa kitongoji cha Matunya, Rodgers Makamba alisema kuwa wakulima zaidi 40 wa kitongoji hicho walilazimika kupanda juu ya miti ili kunusuru maisha yao baada ya kuvamiwa na mafuriko majira ya alfajiri April 6 mwaka huu kufuatia mvua kubwa kunyesha kwa masaa 24 mkoani hapa.
Makamba alisema kuwa alipata taarifa ya mafuriko kuvamia wakulima hao katika bonde la Dutumi ambalo lipo jirani na mto Dutumi majira ya saa asubuhi na kuanza kazi ya kutafuta watu katika miti na kuwapandisha mmoja baada ya mungine hadi nchikavu na zoezi hilo lilidumu kwa muda wa masaa manne ambapo zoezi lilikuwa ngumu kutokana na kuwa na mtumbwi mmoja hali iliyopelekea zoezi hilo kuwa gumu.
“Wakulima zaidi ya 40 katika kitongoji cha Matunya wamekumbwa na mafuriko na walilazimika kupata juu ya miti kwa zaidi ya masaa nne ili kujinusuru na kifo baada ya mafuriko hayo kutokea kwani walifanya hivyo kwa sababu hakukuwa na njia nyingine ya kujiokoa zaidi ya kupata juu ya miti kwani maji hayo yalikuwa na kasi na nguvu sana na baadaye tuliwaokoa kwa mtumbwi na kuwavusha nchikavu”. Alisema Makamba.
Naye Diwani wa kata ya Bwakila Chini, Pesa Mahamedi alisema kuwa mpaka sasa katika kata hiyo kuna uharibifu wa mali uliosababishwa na mafuriko hayo ikiwemo mimea ya mazao mbalimbali ya mpunga, ufuta, mtama na mahindi huku nyumba zaidi ya nyumba 25 nazo zikiwa zimebomoka katika kata hiyo.
Mohamed alisema kuwa kuna maelekezo ya mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi yanafanyiwa kazi baada ya kutembelea na kuona uharibifu huo na kututaka kufanya tathimini ya uharibifu wa mali kupitia kamati za maafa za vijiji na kata ambazo hivi sasa timu hizo zinafanya kazi.
“Tayari mkuu wa wilaya ya Morogoro na mbunge wa jimbo la Morogoro kusini wametembelea katika maeneo yaliyoadhirika na mafuriko na maagizo ambayo tumepewa madiwani wote ni kusimamia kamati za maafa za kufanya tathimini ya uharibufu wa mali iliyotokana na mafuriko hayo”. Alisema Mohamed.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi, Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini na viongozi wa chama na serikali walifanya ziara baadhi ya vijiji vilivyokumbwa ambapo mafuriko hayo yamevikumba vijiji vya kata ya Mvuha, Bwakila Chini, Mngazi na Kisaki na kuharibu nyumba, mimea na mifugo.
No comments:
Post a Comment