Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akisoma jarida la Eagle alilopewa Zawadi na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati
John (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Jumla ya wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini
Nigeria wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.
…………………………………………………………….
NA MAGRETH KINABO
ELIMU
ya uzalendo imesaidia kuwafanya vijana wa Kitanzania kuipenda nchi
yao , hali iliyochangia nchi yetu kuwa na amani na utulivu.
Kauli
hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana
,Utamaduni na Michezo,Seth Kamuhanda wakati akizungumza na ujumbe wa
watu 22,baadhi yao ni viongozi wa utawala na 13 ni wanafunzi wa Chuo cha
Ukamanda na Unadhimu wa mafunzo ya kijeshi kutoka Nigeria.
Ujumbe
huo umetembelea wizara hiyo kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali
ya Utamaduni wa Kitanzania, umeongozwa na kiongozi wa msafara, Meja
Generali, Ati John,ambaye ni Mkurugenzi wa Jeshi la Wanamaji.
“Mojawapo
ya program tunazowafundisha vijana ili kuondoa migogoro katika nchi
yetu ni elimu ya uzalendo ,yaani tunawafundisha jinsi ya kuipenda nchi
yao. Elimu hii imesaidia kupunguza migogoro,alisema.” Katibu Mkuu huyo
alipokuwa akijibu swali la mmoja ya wanafunzi hao lililouliza kuwa
kuna program zipi zinazochangia kupunguza migogoro hususan kwa
vijana.
Katibu
Mkuu huyo aliongeza kuwa kuna mkakati wa kuwawezesha vijana kiuchumi
ili waweze kubuni miradi mbalimbali kwa kuwa na mfuko wa vijana.
Alisema katika mpango huo vijana wanakuwa katika vikundi na kufanya shughuli mbalimbali kuwawezesha kiuchumi.
Aidha
Katibu Mkuu huyo akizungumza kuhusu masuala ya kiutamaduni ,alisema
wizara yake ndi yenye jukumu lakuendeleza Utamaduni wa Mtanzania, hivyo
katikawizara hiyo yenye sekta nne, ambazo ni Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo.
Kamuhanda alisema sektaya utamuduni ndio inayofanyakazi ya kudumisha Utamaduni huo.
Aliongeza kuwa lugha ya Kiswahili ndio imekuwa lugha kuu ya mawasiliano nchini na ndiyo iliyoleta umoja ,amani na mshikamano.
Wakizungumzia
kuhusu ziara hiyo kiongozi huyo na mmoja wa wanafunzi, Ikema Francis
walisema wameshukuru kwa taarifa walizopata kuhusu wa masuala hayo ya
kiutamaduni na kuhafamu kuwa lugha ya Kiswahili ndiyo imeleta umoja.
No comments:
Post a Comment