Na Benedict Liwenga, Maelezo, Dodoma.
Jumla shilingi bilioni 54.4 zimepatikana zimepatikana kutokana na ushuru kwa mauzo ya mazao ya samaki hapa nchini.
Takwimu
hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, Mhe. Benedict Ngalama Ole-Nangoro wakati akijibu swali
la Mbunge wa Jimbo la Wawi, Mhe. Hamad Rashid Mohamed aliyetaka kujua
katika kipindi cha mwaka 2005 hadi2012 Tanzania imesafirisha tani ngapi
za mazao ya Samaki kutoka Bahari Kuu na Maji baridi (Maziwa), na Meli
ngapi za uvuvi wa Bahari Kuu zilipewa leseni na zilisafirisha tani ngapi
za Samaki kwa thamani gani na je Serikali imepata mapato kiasi gani kwa
kutoza kodi za aina gani.
Amesema
kati ya mapato hayo shilingi bilioni 5.5 ni kutoka maji chumvi na
bilioni 48.9 zilitokana na samaki wa ziwani au maji baridi.
Mhe.
Ole-Nangoro amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012,
Tanzania imesafirisha jumla ya tani 371,317.8 za samaki na mazao ya
uvuvi ambapo tani 17,954.5 ni kutoka maji chumvi na tani 353,362.7
kutoka maji baridi ambapo Ziwa Victoria ni 339,893.1, Tanganyika
11,418.8, Nyasa 110.9 na maeneo ya maji madogo ni 1,939.9 pamoja na
Samaki hai 301,839.
Aidha,
ameongeza kuwa kati ya mwaka 2005 hadi 2009, jumla ya leseni 274
zilitolewa na Tanzania bara kwa ajili ya uvuvi katika bahari kuu.
“Kabla
ya mwaka 2009, wakati Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu kuanzishwa, Tanzania
Bara na Tanzania Zanzibar zilikuwa zinatoa leseni kila mmoja kwa ajili
ya uvuvi katika bahari kuu”. Mhe. Ole-Nangoro alisema.
Amesema kuwa baada ya kuanzishwa Mamlaka hiyo, kati ya mwaka 2010 hadi 2012 jumla ya leseni 124 zilitolewa.
Aidha
, Naibu Waziri huyo amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012
jumla ya meli 398 zilipewa leseni za uvuvi wa Bahari Kuu, ambapo Meli
zote zilizopewa leseni hizo zilivua jumla ya tani 40,081.8 za samaki
ambazo zilisafirishwa na kuuzwa nje ya nchi.
Katika
hatua nyingine Serikali imesema kuwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012
,jumla ya shilingi bilioni 12.6 zimepatikana kutokana na ada ya leseni .
No comments:
Post a Comment