Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hotuba wakati wa harambee ya kutunisha
mfuko wa kuwasaidia wajasiliamali wadogo na wananchi wanaoishi Jimbo la
Ukonga kuwainua kimaendeleo.
Bendi
ya muziki, The Babloom Trio ikitoa burudani wakati wa kuchangia mfuko
wa kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wananchi wanaoishi Jimbo la Ukonga
kuwainua kimaendeleo. kushoto Mkurugenzi wa bendi hiyo Bw.Seif Kisauji
pamoja na wanamziki wengine.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimsikiliza Mbunge
wa jimbo la Ukonga Mhe.Eugen Mwaiposa wakati akitoa hotuba yake( wapili
kushoto kwake) Mwenyekiti wa Ukonga SACCOS Bi.Adivela Ruge
akitoa hotuba wakati wa harambee ya kutunisha mfuko wa kuwasaidia
wajasiliamali wadogo na wananchi wanaoishi Jimbo la Ukonga kuwainua
kimaendeleo.
Diwani kata ya Kipawa Mhe Bonnah Kaluwaa (katikat)kiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wake.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
RAIS
Jakaya Kikwete ameongoza harambee ya kutunisha mfuko wa kuwasaidia
wajasiriamali wadogo na wananchi wanaoishi Jimbo la Ukonga jijini Dar es
salaam kuwainua kimaendeleo.
Katika
harambee hiyo iliyofanyika jana kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam na kuudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Wilaya ya
Ilala, jumla ya sh. mil 462 zilikusanywa ikiwa ahadi na fedha taslimu
huku Rais Kikwete akichangia mil 5.
Rais
Kikwete akizungumza katika harambee hiyo alitoa pongezi kwa mbunge wa
jimbo hilo Eugen Mwaiposa kwa kuandaa mkakati huo ambao kama utasimamiwa
vema utasaidia kuinua vipato vya wafanyabiashara wa wadogo na wananchi
wenye hali duni ya kuendesha maisha yao.
Moja
ya lengo la harambee hiyo ni kuanzisha SACCOS ambayo itatumika na
wafanyabishara wadogo sanjari na wananchi kukopa na kutunisha mitaji yao
ya biashara ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
”Nimefurahishwa
na malengo ya kufanya harambee ili kupata fedha zitakazosaidia
kuanzisha SACCOS ambayo ni moja ya Ilani yetu, lakini pia nimejisikia
faraja zaidi kuniambia mkakati wenu mwingine ni kuifanya kuwa benki ya
Wananchi,”.Alisema Kikwete.
Aliongeza
kuwa Serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu katika fani mbalimbali
huku akisisitiza kuwa ajira nyingi zinazopatikana Serikalini ni walimu
na madaktari lakini kwa sekta nyingine hakuna nafasi za kutosha.
Hivyo
alitoa mwito kwa vyuo vya ufundi Stadi kutoa mafunzo yanayohitajika
kwenye soko la ajira ambayo pia yatakayotoa fursa kwa vijana kujiajiri
wenyewena kuwaajiri wenzao sanjari na kuwataka vijana kuhakikisha
wanachukua mafunzo yatakayowatia ajira kwa uraisi.
Mbunge wa Jimbo hilo, Mwaiposa alisema eneo lake wakazi asilimia 92 ni
wajasiriamali wadogo ambao baadhi yao wamo katika nyanja ya Ufugaji na
biashara nyingine na wameshindwa kufikia mafanikio kutokana na kuwa na
mitaji midogo.
Aliongeza
kuwa harambee hiyo ina malengo matatu moja likiwa ni kuwaondolea
changamoto zinazowakabili kwa kuanzisha Saccos na kuendeleza Vikoba 54
vilivyopo sasa kati ya 104 vilivyopo awali.
Pili
alisema kuwa ni kutoa elimu ya biashara na kutafuta masoko hali ambayo
itasidia kufikia malengo katika shughuli zao za ujasiliamali sanjari na
kuondoa matatizo ya maji ambayo ni kero kubwa kwa wananchi wa huko.
Kabla
ya harambee hiyo iliyofanyika juzi, Jimbo hilo lilikuwa na mtaji wa
mil. 26 zilizotokana na vikundi 128 vya vikoba na mahitaji yalikuwa ni
kupatikana Sh. mil 600.
Licha
ya Rais Kikwete kufanya jitihada kubwa ya kuchangisha fedha
zilizopatikana wengine waliochangia ni Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Concept,
Juma Pinto ambaye alitajwa kuchangia Sh. mil 4 japo hakuwepo katika
halfa hiyo na kupongezwa na mkuu huyo wa nchi.
”Namshukuru
Pinto kwa mchango wake wa kuchangia maendeleo ya jimbo la Ukonga na
aendelee kuwa na moyo huo ili kukoa vijana katika dimbwi la ukosefu wa
ajira”alisema Kikwete.

No comments:
Post a Comment